WAKATI Vifaa vya uchaguzi vikiwasili Visiwani Zanzibar kwa ajili ya kutumika katika marudio ya uchaguzi visiwani humo,hadi sasa Wagombea wa uwakilishi katika majimbo 16 Zanzibar kupitia Chama cha CUF hawajachukua fomu na bado wameazimia kutoshiriki uchaguzi huo wa marudio visiwani humo unaotarajia kufanyika Machi 20 mwaka huu.
"Kutokana na msimamo huo lakini wapo baadhi ya wawakilishi ambao wamesikikia wakilalama vipembeni kuwa wamepata hasara katika uchaguzi wa awali uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana, ambapo wanatamani kushiriki uchaguzi huo ili waweze kurejesha fedha zao walizotumia katika uchaguzi wa awali,
''Unajua Politics ndio maisha yao, walitumia hela nyingi uchaguzi wa Oktoba 25, na wengine hadi sasa bado wanajiamini kushinda japo warudishe fedha zao walizo investi na endapo CUF wanataka wasishiriki uchaguzi, basi waandae mkakati wa kuwalipa pesa sawa na ambazo wangepata wakiwa wawakilishi. alisema mkazi mmoja wa Chukwani aliyejitambulisha kwa jina la Kijeshi
Sehemu ya Vifaa hivyo baada ya kushushwa mjini Zanzibar leomchana.




No comments:
Post a Comment