Basi la City Boy likiwa katika mwendo mkali kabla ya kupata ajali na kuuwa watu eneo la Manyoni Mkoani Singida leo mchana. Imeelezwa kuwa katika ajali hiyo jumla ya watu 27 wamefariki dunia papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Basi hilo baada ya kupinduka kichwa chini miguu juu.
***************************
Akizungumza na Mtandao huu kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Thobias Sedoyeka, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea majira ya saa nane mchana wa leo, ambayo ilihusisha mabasi ya Kampuni moja ya CITY BOYS, moja lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kwenda Kahama na jingine likitokea Kahama kuelekea jijini Dar es Salaam.
Aidha baadhi ya mashududa wa ajaili hiyo pia walielezea uzoefu wao kuhusu madereve wa mabasi ya kampuni hiyo, ambapo walisema kuwa madereva hao mara kadhaa wanapokutana na kupishana hupishana kwa mbwembwe huku kila mmoja akipita upande wa mwenzake huku wakiwa katika mwendo mkali kama ishara ya kusalimiana.
Hawa madereva wa mabasi ya kampuni hii mara kadhaa huwa wamekuwa wakiwashangaza abiria wao kwa stali ya kupishana pindi wanapokutana huwa kila mmoa hupita upande wa mwenzake tena kwa speed ile ile'' alisema mzoefu mmoja aiyekuwa eneo la tukio, ambaye hakupenda jina lake liandikwe.
Moja ya basi hilo likiwa chakari baada ya ajali hiyo. PICHA NYINGINE ZINATISHA NA PIA KULINGANA NA MAADILI YA HABARI TUMESHINDWA KUZICHAPISHA.




No comments:
Post a Comment