BEKI wa Manchester United, na timu ya Taifa ya Uingereza, Chris Smalling ameshonwa nyuzi tatu katika paji lake la uso juu ya jicho la kulia baada ya kuanguka na kuumia wakati akiwa mapumzikoni huko mjini Bali.
Imeelezwa kuwa Smalling amekutwa na kadhia hiyo wakati akiwa na mpenzi wake, Sam Cooke, kwenye kisiwa cha Indonesia wakiwa mapumzikoni, ambapo baada ya tukio hilo alikimbizwa hospitali na kupatiwa matibabu.
Beki huyo baada ya kikosi chake cha Taifa kuondolewa kwenyw michuano ya Euro 2016 yupo mapumzikoni kabla ya kujiunga na wenzake katika kikosi kipya cha kocha mpya Jose Mourinho, kwa ajili ya ziara ya China kujiandaa na msimu mpya ujao.
Aidha habari kutoka Uongozi wa Manchester United zinasema kuwa beki huyo, baada ya kuanguka alipoteza fahamu na kuangukia kichwa, baada ya kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu.
Tayari Smalling ameruhusiwa na Madaktari kuondoka hospitali na amerejea kuendelea na mapumziko yake na atawasili Carrington baadaye mwezi huu kama ilivyopangwa.
No comments:
Post a Comment