Na: Frank Shija, MAELEZO
Serikali imeipongeza Benki ya Standard
Chartered Tanzania kwa kupeleka huduma za kibenki kwa wananchi wanao ishi
katika maeneo ambayo benki hiyo haina matawi hapa nchini.
Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa.Makame Mbarawa katika hafla fupi ya
Iftari iliyoandaliwa na Benki hiyo jana Jijini Dar es Salaam.
Mbarawa amesema kuwa Sekta ya Benki ni
muhimu kwa jamii hivyo kwa Standard Chartered Tanzania kupeleka huduma zao
kupitia ushirikiano baina yao na Benki ya Posta katika matawi yake pote nchini.
“Nawapongeza sana kwa kuona haja ya
kushirikiana na Benki ya Posta ili kuwapelekea huduma wananchi wengi zaidi
katika maeneo ambapo hamna matawi yenu.”Mbarawa.
Aidha Mbarawa alitumia fursa hiyo
kuwata Waumini wa dini ya Kiislamu na wananchi kwa ujumla kuwa na mahusiano
mema ili kudumisha amani.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa
Benki ya Standard Chartered Tanzania Sanjay Rughani amesema kuwa Benki yao
imeona umuhimu wa kupanua wigo wa huduma zao kutokana na kuwa na matawi
machache nchini nzima.
Aliongeza kuwa uamuzi huo umefikiwa
baada ya kusikia uhitaji wa wananchi hususan wakazi wa Arusha ambao waliomba
kuongezewa matawi ya Benki hiyo kutoka tawi moja lililopo sasa.
Benki ya Standard Chartered Tanzania
imeingia ubia na Benki ya Posta Tanzania ili kutoa huduma za kibenki kupitia
matawi ya Benki ya Posta popote yalipo nchini na kwa kufanya hivyo kunatoa
fursa kwa wananchi wengi zaidi kunufaika na huduma za Benki ya Standard
Chartered Tanzania.

No comments:
Post a Comment