Na
Daudi Manongi, MAELEZO
Mamlaka
ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kuwa sikukuu za Eid al
Fitr na Sabasaba zilisababisha ukosefu wa nishati ya Petroli Mkoa wa Mtwara na
kuathiri wa baadhi ya shughuli za maendeleo.
Hatua
hii ilitokana na wamiliki wengi wa ‘deport’ za mafuta kufunga kwa ajili ya
kushiriki sikukuu hizo.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Meneja
Mawasiliano na Uhusiano (EWURA) Bw.Titus
Kaguo wakati wa mahojiano na Idara
ya Habari(MAELEZO) wakati akitoa ufafanuzi
juu ya uhaba wa tatizo hilo katika Mkoa wa Mtwara lililoripotiwa na baadhi ya
vyombo vya habari.
Alisema
kuwa hivi sasa hali ya upatikanaji wa nishati hiyo imerejea kwani vituo vingi
vimeanza kuuza nishati hiyo baada ya sikukuu hizo kumalizika.
Bw.Kaguo
alisema kuwa kutokana na biashara hiyo kuendeshwa na watu binafsi na wahusika
hao kushiriki sikukuu hiyo ilisababisha kusimama kwa shuguli hiyo, hatua
ilivifanya baadhi ya vituo kukosa nishati ya mafuta na kushindwa kufanya kazi
katika kipindi hiki cha sikukuu.
Aidha
amewahakikishia wananchi kuwa kwa sasa nishati ya Petroli na Dizeli
ipo kwa wingi kwani kwa siku ya jumanne dizeli lita milioni (5) tano ziliuzwa ukilinganisha
na matumizi ya nchini ya siku ambayo ni lita milioni 4.8 na kwa Petroli lita zilizouzwa
ni milioni 3.6 ukilinganisha na matumizi ya nchi nzima ya petroli ya lita
milioni 2.8. kwa siku.
Aliongeza
kuwa toka jumanne vituo kama Lake Oil,Tsn na Central belt vimeendelea kutoa
huduma kama kawaida kwa wananchi wa Mkoa wa Mtwara.
Mji
wa Mtwara siku ya Jumatano ulikumbwa na uhaba wa mafuta ya Petroli na hivyo
kufanya wakazi wa mji huo kununua nishati hiyo kwa bei ya ulanguzi toka lita shilingi
1950 hadi kufikia shilingi 2500 kwa lita jambo liloathiri shughuli za maendeleo
ya wananchi.

No comments:
Post a Comment