Baadhi ya Sehemu za Uzalishaji ndani kiwanda hicho ambayo yanalalamikiwa na Wanachi kwa Uzalishji vumbi linalowaathiri wananchi.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akizungumza na Uongozi wa kiwanda cha twiga cement,pamoja na Maafisa kutoka Baraza la Usimamizi wa Mazingira(NEMC)alipofanya ziara mapema hii leo.
Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh,luhaga Mpina (katikati) na Meneja mazingira kiwandani hapo bw. Richard Magoda akitembezwa ndani ya kiwanda baada ya kupata malalamiko ya uchafuzi wa mazingira kutoka kwa wananchi.
*********************************
Kiwanda cha kutengeneza cement cha
Twiga cement cha wazo jijini dar es Saalaam kimepewa muda wa mwezi mmoja
kurekebisha mfumo wao wa utoaji taka ili kunusuru uharibifu wa mazingira na
maisha viumbe hai.
Hayo yamesemwa Leo jijini Dar es
Salaamna waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.
Luhaga Mpina katika ziara yake ya kutembelea kiwanda hicho.
Mhe. Mpina amekitaka kiwanda
hicho kushirikiana na Baraza la Taifa la
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC kupima vumbi litokanalo na uzalishaji
kiwandani.. ili kuona kama ni la kiwango ambacho si hatarishi kwa mazingira na
viumbe hai vinavyozunguka maeneo hayo.
Maagizo hayo ya Naibu waziri Mpina
yametokana na malalamiko ya wananchi wa maeneo jirani na kiwanda hicho
yanayoeleza kuwa kiwanda hakina mahusiano mazuri na wakazi au majirani wa
maeneo hayo hivyo, amemtaka muwekezaji huyo kuimarisha mahusiano baina ya
kiwanda hicho na wananchi na kufanyia marekebisho kasoro zilizoonekana
kujitokeza kiwandani hapo na kuwaasa wawekezaji wa kiwanda hicho kufanya kazi
pamoja na kuheshimu sheria hususan za mazingira.
Kwa upande wa Baraza la Taifa na Usimamizi
wa Mazingira Nemc kumeonekana kuwa na uzembe katika ufuatiliazi wa utekelezaji
wa sheria za mazingira hasa kiwandani hapo, baada ya mkurugenzi wa uzingatiaji
na utekelezaji wa baraza hilo bi Ruth Lugwisha kushindwa kujibu swali
aliloulizwa na Naibu waziri Mpina kuwa ni lini Mara ya mwisho baraza hilo
lilijiridhisha kwa kuchukua vumbi kiwandani hapo na kulipima ili kujua lina
athari kwa kiasi gani kwa mazingira na viumbe hai.
Kwa upande wake Meneja wa Mazingira
wa kiwanda hicho Bw. Bw. Richard Magoda amejitetea kuwa kiwanda kina mahusiano
mazuri na wanachi kwani kimeweza kutoa misaada katika baadhi ya maeneo ikiwa ni
pamoja na vyandarua na kuchonga barabara za baadhi ya mitaa.
Wakati huo huo viongozi wa serikali
za mitaa Bw. Gration Mbelwa (mwenyekiti
wa kata ya madale) na Atilio Maginga
mwenyetiki wa serikali ya mtaa wa mivumoni..wametofatofautiana kwa kusema kwamba kiwanda kina mashirikiano
mazuri na wananchi, wakati mwenyekiti wa kata ya madale akiwakilisha wanachi
kwa kulalamika kuwa kiwanda hakina mahusiano mazuri na wananchi..



No comments:
Post a Comment