Habari za Punde

*MSANII WA VICHEKESHO KUNDI LA VITUKO SHOO 'KUNDAMBANDA' AFARIKI DUNIA

Msanii maarufu wa Vichekesho (Komedi)  kutoka  kundi la Vituko Show Ismail Issa Makombe almaarufu kama 'KUNDAMBANDA', amefariki dunia usiku wa kuamkia jana.
Kundambanda alikuwa mgombea ubunge wa CUF na UKAWA kwenye jimbo la Masasi - Mtwara katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Disemba 2015 baada ya ule wa Oktoba kutofanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea wa awali wa UKAWA, Mhe. Emmanuel Makaidi (NLD). 
Katika uchaguzi huo wa Disemba 2015 Kundambanda alipata kura 14,069 dhidi ya kura 16,597 za (mshindi) Rashid Chua Chua kutoka CCM. 
Taratibu za mazishi zinafanyikia nyumbani kwao Masasi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.