Habari za Punde

*NAIBU WAZIRI WA HABARI ANASTAZIA ATEMBELEA ENEO LITAKAPOJENGWA KITUO CHA MAFUNZO YA MICHEZO

 Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akionyeshwa eneo litakalo jengwa kituo cha mafunzo ya michezo leo  jijini Arusha leo na Katibu Mkuu wa Trust St.Patrick Sport Academy Bi.Dinna Patrick alipotembelea eneo hilo kujionea hali halisi.
 Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura(katikati) akitoa maagizo leo jijini Arusha kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa Bi Alice Mapunda(wakwanza kushoto) kuhusu barabara iliyopita katikati ya mradi huo  wa kituo cha mafunzo ya michezo.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Annastazia Wambura akisalimiana na Mwanariadha wa zamani Bw.Faustine Sulle ,mara baada ya mkutano wa wadau wa kisekta uliyofanyika jijini Arusha katika ofisi za Mkuu wa Mkoa.
 Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Annastazia Wambura (watano kushoto) akiwa katika picha ya pamoja leo jijini Arusha na baadhi ya wanafunzi wa wasichana katika Shule ya Trust St.Patrick Sport Academy wanaocheza mpira wa alipotembelea shule hiyo inayofundisha michezo mbalimbali ,wanne kulia ni Meneja wa Shule hiyo Bw.Patrick Khagya.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Annastazia Wambura (watano kushoto) akiwa katika picha ya pamoja leo jijini Arusha na baadhi ya wanafunzi wa wanaocheza mpira wa kikapu katika Shule ya Trust St.Patrick Sport Acadealipotembelea leo jijini Arusha  kujionea timu zao za michezo,watatu kushoto ni Katibu Mkuu wa Shule Bi.Dinna Patrick. Na Anitha Jonas – MAELEZO,ARUSHA
**************************************************
Anitha Jonas – MAELEZO
Serikali ya pongeza uongozi wa Trust St.Patrick Sport Academy  kwa uamuzi wa kujenga  Kituo cha Mafunzo ya Michezo chenye hadhi  ya Kimataifa.
Pongezi hizo zimetolewa leo jijini Arusha na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipotembelea eneo hilo litakalojengwa kituo hicho ambacho kitakuwa na Michezo ya aina mbalimbali pamoja na hoteli ya nyota tano.
“Serikali inaunga mkono jitihadi za ujenzi huu kwani kituo hichi kitakapo malizika tunaimani kitakuwa chachu  ya ukuaji wa vipaji vya michezo kwa watanzania na kutaongeza mafanikio ya sekta ya michezo na kuwezesha kupata ushindi katika michezo mbalimbali katika ngazi za Kimataifa,”alisema Naibu Waziri.
Naye Katibu Mkuu wa Kituo hicho Bi.Dinna Patrick  alimweleza Naibu waziri huyo chagamoto waliyonayo  katika eneo hilo la kuwepo kwa barabara inayogawa eneo hilo la kituo hicho ambalo ndiyo limekuwa kikwazo kinacho kwamisha ujenzi wa kituo hicho kuanza kwa haraka.
“Kituo hicho kitakuwa na uwanja wa mpira ambao utakuwa na uwezo wa kuchukua watu elfu ishirini ambao utakuwa wenye hadhi ya kimataifa na kituo hicho kinatarajiwa kuwa bora zaidi katika Kanda ya  Afrika Mashariki”,alisema Bi.Patrick.
Baada ya kupata malalamiko hayo Mheshimiwa huyo aliuagiza uongozi wa mkoa  kufuatilia suala hilo katika ofisi za Halimashauri na kusaidia suala hilo kupata ufumbuzi ili kuharakisha ujenzi wa eneo hilo kwani kumalizika kwake kutaleta faida kubwa  kwa wapenzi wa michezo.
Aidha ,Naibu waziri huyo alitoa wito kwa uongozi wa Trust St.Patrick Sports Academy kujenga pia chuo cha walimu wa michezo mbalimbali nchini kwani kuna changamoto kubwa ya ukosefu wa walimu wa michezo na uhaba wa vyuo vya michezo nchini.
Hata hivyo watanzania wenye uwezo wametakiwa kujitokeza na kujenga vituo vya mafunzo ya michezo kwani michezo ni ajira na inaweza kuchangia pato kubwa katika nchi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.