Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akiwasili katika Eneo la Ghana tayari kwa ukaguzi wa barabara inayopanuliwa na kujengwa kwa lami kwa kiwango cha Km 2.7.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella, akitoa maelekezo kwa Mtaalaam mshauri, namna gani wafanye ili kuweza kuepusha athari ya mafuriko pindi mvua zitakapo nyesha.
Moja ya Mainjinia wa Nyanza Roads works, alipokutwa kazini, wakati wa ziara ya Mhe, John Mongella Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kwenye ukaguzi wa barabara hiyo.
Mhandisi wa Maji mjini Mwanza, Mhandisi Sanga, akitoa maelezo kwa waandishi wa habari namna walivyo tekeleza, maazimio yakuhamisha miundo mbinu ya maji ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo ya makongoro.
Mhe. John Mongella Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akiongea na waandishi wa habari mara baada yakufanya ziara ya kukagua barabara ya Makongoro Uwanja wa Ndege inayopanuliwa na Mkandarasi Nyanza Road ya Jijini Mwanza na kutoa maelekezo yakuikabidhi barabara hiyo ifikapo Novemba, 2016. Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
**********************************
**********************************
TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO VYA
HABARI
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella, ametembela na kujionea upanuzi wa wa barabara ya Uwanja wa
Ndege Mwanza na kisha kuwawataka
wananchi kuwa tayari kutoa ushirikiano kwa Serikali pindi inapohitaji kufanya
shughuli za maendeleo.
Akiwa
katika Eneo la Upanuzi wa barabara hiyo eneo la Ghana, amewapongeza wananchi
wote waliotoa ushirikiano katika awamu ya kwanza kwakukubali kuondosha shughuli
zao ambazo zilikuwa pembezoni mwa hifadhi ya barabara ili kupisha upanuzi
unaofanyika hivi sasa wa Km. 2.7 kuanzia eneo la Ghana hadi Pasiansi
Katika
hatua Nyingine Mongella amemuagiza Mkandarasi kuhakikisha anamaliza kazi hiyo
kwa wakati ili kuondosha msongamano wa magari ambao umekuwa ni kero kwa
wananchi hasa nyakati za asubuhi na jioni,
Aidha Mongella, ameahidi kufanya ziara kila baada ya wiki mbili ili
kujionea maendeleo ya barabara hiyo na kusema ifikapo Novemba 26 mwaka huu
Mkandarasi awe amekabidhi kazi hiyo.
Upanuzi
wa barabara hiyo Unafatia maamuzi yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli, kwa kuagiza kiasi
cha fedha Bil.2.7 zilizokuwa zimetengwa kwaajili ya Sherehe za Muungano
kubadilishiwa matumizi na kupelekwa
kwenye upanuzi wa barabara hiyo ili kuondoa adha ya msongamano wa magari kwa
wananchi husan ni wale wanao tumia barabara ya Uwanja wa Ndege.
Imetolewa na
Atley J. Kuni
Afisa Habari na Uhusiano- RS
Mwanza
13. Julai, 2016





No comments:
Post a Comment