Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akigonganisha
bilauri na Mke wa Rais wa Rwanda, Mama Jeannette Kagame katika kusherehekea Dhifa ya Kitaifa aliyomuandalia mgeni wake Rais
wa Rwanda Paul Kagame (katikati) Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais Kagame
alikuwa nchini kwa ziara ya Kikazi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (kulia) akigonganisha
bilauri na Rais wa Rwanda Paul Kagame, katika kusherehekea Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt. John
Pombe Magufuli kwa ajili ya mgeni wake Rais Kagame. Dhifa hiyo ilifanyika Ikulu
jijini Dar es Salaam jana usiku.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akiwa
amesimama kutoa heshima wakati wa Dhifa ya Kitaifa aliyomuandalia mgeni wake Rais Kagame (kulia kwake). Kulia ni
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan. Wa pili kulia ni Mke wa Tanzania Mama Janet
Magufuli na kushoto ni Mke wa Rais wa Rwanda, Jeannette
Kagame.
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa tatu kushoto) akiwa na
Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim (wa pili kushoto), Jaji Mkuu wa
Tanzania Mohamed Chande Othman (wa tatu kulia) Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine
Mahiga na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Louise Mushikiwabo (kulia).
Waziri Mkuu Mstaafu Jiji Mstaafu Joseph Sinde
Warioba akimsikiliza Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri Dkt. Tulia Ackson wakiwa
kwenye Dhifa ya
Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa mgeni wake Rais
Kagame. Dhifa hiyo ilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. KWA PICHA ZAIDI BOFYA READ MORE
Jaji Mkuu
wa Tanzania, Mohamed Chande Othman
(kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani
Madabida wakiwa kwenye Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt. John Pombe
Magufuli kwa ajili ya mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame aliyetembelea
Tanzania kwa ziara ya Kikazi.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi (kushoto) akiwa na Spika Mstaafu Anne Makinda (kulia), wakimsilikiza Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage.
Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeir (kushoto)
akizungumza na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Alhad Musa Salum (katikati).
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kwenye Dhifa ya Kitaifa aliyoiandaa kwa ajili ya mgeni
wake Rais wa Rwanda Paul Kagame (kulia) Ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku. Katikati
nini Mke Kagame, Mama Jeannette Kagame.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kwenye
Dhifa Dhifa ya
Kitaifa aliyoiandaa kwa ajili ya mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame (wa tatu
kushoto) Ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku.
Kulia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
anayemfuatia ni Mke wa Rais wa Tanzania mama Janet Magufuli na wa pili kulia ni
Mke Kagame, mama Jeannette
Kagame.
Rais wa Rwanda Paul Kagame akizungumza kwenye Dhifa Dhifa ya Kitaifa aliyoiandaliwa na mwenyeji wake Rais Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (wa tatu kushoto). Kulia ni Mke wa Rais wa Tanzania, mama Janet Magufuli na wa pili kushoto ni Mke Kagame, mama Jeannette Kagame.
Baadhi ya waalikwa waliohudhuria Dhifa ya Kitaifa
iliyoandaliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa mgeni wake Rais wa Rwanda
Paul Kagame, Ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku, wakimsikiliza Rais Kagame
(hayupo pichani).
Rais wa Rwanda Paul Kagame akimsalimia Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi. Katikati ni Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim.Kushoto ni Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (wa pili kushoto)
akimtambulisha Balozi wa China Nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing kwa
mgeni wake Rais wa
Rwanda Paul Kagame.
1.
Rais wa Rwanda Paul Kagame (kulia) akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri
Dkt. Tulia Ackson.Kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu Jiji Mstaafu Joseph Sinde
Warioba.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, akimtambulisha Spika Mstaafu Anne Makinda kwa mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, akiwa na mgeni wake
Rais wa Rwanda Paul Kagame,
wakiangalia burudani ya kikundi cha Matarumbeta.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi wakati wakiondoka kwenye
ukumbi wa Ikulu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, akimsikiliza Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim (katikati) wakati
wakiondoka kwenye ukumbi wa Ikulu.Wa pili kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu Jiji Mstaafu Joseph Sinde Warioba na kulia ni Mke
wa Rais Mama Janet Magufuli. Picha na Hussein
Makame-MAELEZO
No comments:
Post a Comment