Mwakilishi wa Shirika la Watoto
Duniani(UNICEF) Bi.Cecilia Baldeh akieleza jambo wakati wa uzinduzi wa matokeo ya utafiti wa
utumikishwaji wa watoto wa mwaka 2014 Tanzania Bara uliofanyika katika ukumbi
wa Wizara ya Fedha na Mipango leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt
Albina Chuwa akitoa maelezo mafupi kuhusu ripoti ya matokeo utafiti wa
utumikishwaji wa watoto wa mwaka 2014 Tanzania Bara uliofanyika katika ukumbi
wa Wizara ya Fedha na Mipango leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira
na Walemavu Dk. Abdallah Possi akizungumza kabla hajazindua matokeo ya utafiti wa utumikishwaji wa watoto
wa mwaka 2014 Tanzania Bara uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango
leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Dk. Abdallah Possi akionyesha ripoti
ya matokeo ya utafiti wa utumikishwaji
wa watoto wa mwaka 2014 Tanzania Bara mara baada ya kuizindua leo jijini Dar es
Salaam.Kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Kazi Dunia Tanzania Bw,Jealous
Chirove.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Dk. Abdallah Possi akimkabidhi ripoti
ya matokeo ya utafiti wa utumikishwaji
wa watoto wa mwaka 2014 Tanzania Bara mwakilishi wa Shirika la kazi Duniani,Geneva
Bw.Azfar Khan leo jijini Dar es Salaam.
******************************************************
Na Daudi Manongi,MAELEZO
Serikali imesema kuwa itaendelea
kupambana na kupinga utumikishwaji wa watoto nchini ili tuwe na Taifa imara.
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Dk.Abdallah Possi alipokuwa akizindua ripoti
ya matokeo ya utafiti wa utumikishwaji wa watoto wa mwaka 2014 Tanzania Bara
Jijini Dar es Salaam ambayo imeonyesha kuwa utumikishwjai wa watoto umepungua
kutoka asilimia 30.1 mwaka 2006 mpaka asilimia 28.8 mwaka 2014.
Dk Possi alisema kuwa Jitihada
mbalimbali zinaendela kufanywa na serikali ya awamu ya Tano ikiwemo utoaji wa
Elimu bure ili kuhamasisha mahudhurio ya watoto shuleni na kupunguza uwezo wa watoto
kujihusisha na ajira za utotoni.
Aidha Naibu Waziri uyo alisema kuwa utafiti
huo umebaini kuwa takribani watoto milioni 5 wanajihusisha na shughuli za
kiuchumi, miongoni mwao wasichana ni asilimia 52.5 na wavulana ni asilimia 47.5 ambayo kwa
ujumla katika watoto wa tatu mmoja anajihusisha katika shughuli za kiuchumi uku
sekta ya kilimo,misitu na uvuvi ndo zimebeba asilimia 92.1 ya watoto wote
wanaojihusisha na shughuli za kiuchumi.
Aidha ripoti hiyo imeonyesha kuwa
watoto wanaotumikishwa vijijini ni wengi kuliko mijini na hivyo maendeleo ya
kiuchumi ni muhimu katika kuhakikisha ajira kwa watoto zinatokomezwa na kwa
hili serikali inaendelea kuhakikisha kuwa elimu na maendeleo vijijini
yanapatikana ili kuondoa tatizo hilo.
Kwa upande wa elimu ripoti inaonyesha kuwa
watoto wanaoishi mijini hutumia muda mwingi kujisomea tofauti na walioko
vijijini ambapo watoto wanaoishi Dar es Salaam hutumia muda mrefu zaidi katika
kujisomea ambapo ni sawa na asilimia 19.9 ikifuatiwa na maeneo mengine ya mjini
ambao hutumia asilimia 17.8 ya muda wao kwa siku kwa kujisomea na watoto wa
vijijini walitumia asilimia 14.4 kwa ajili ya shughuli za kujisomea.
Naye Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya
Takwimu Dkt Albina Chuwa amesema kuwa ripoti hii itasaidia katika kutengeneza sera
nzuri za maendeleo na kudai kuwa kila mtu ana jukumu la kuhakikisha watoto
wanalindwa na kuacha kutumikishwa katika shughuli za kiuchumi na pia taasisi
yake imejiandaa vyema katika kutumia mfumo mpya na wa kisasa unaoitwa E-popular register ili kupata takwimu
ambazo zinaendana na wakati.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika
la Watoto Duniani(UNICEF) Bi.Cecilia Baldeh amesema kuwa asilimia 29 ya watoto
duniani wanatumikishwa katika shughuli za kiuchumi na hivyo kukosa haki yao ya
msingi ya kusoma na kuiomba serikali kufuatilia kwa karibu mazingira ya kazi
yanayohusisha watoto na kushauri kuwekwa kwa mfumo wa kijamii ambao utasaidia
kufatilia na kuwalinda watoto katika
Nyanja zote.





No comments:
Post a Comment