Na Zainab Nyamka, Dar
TANZANIA imesema lazima itahakikisha inashiriki michuano ya kombe la dunia itakayofanyika mwaka 2026. Mbali na fainali hizo pia imeweka mipango na malengi ya kuisaidia timu ya Taifa ya wanawake kutinga fainali pamoja na ile ya vijana kucheza michuano ya olimpiki itakayofanyika Tokyo mwaka 2020.
Akizungumzia mikakati hiyo, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi alisema kuwa jitihaza zilizopo sasa ni kuhakikisha wanaunda timu bora ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 na katika kuhakikisha hilo linafanikiwa kuanzia mwezi Agosti kutakuwa na Ligi Kuu ya vijana itakayoshirikisha timu B za timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom.
Amesema kuwa kwa mara ya kwanza watahakikisha Tanzania inachaguliwa kucheza michuano hiyo ya olimpiki itakayofanyikia Tokyo. "Kwa kipindi kirefu tumekuwa hatuna timu inayowakilisha vizuri nchi lakini kupitia mpango huu tutahakikisha timu itakayochaguliwa ya U-20 inashiriki michuano hiyo ya Olimpiki". alisema Malinzi
Aidha Malinzi alisema kuwa timu hiyo itakayochaguliwa itaweka kambi nchini Shelisheli mwezi Disemba kwa ajili ya maandalizi pia mwakani wataendesha mashindano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 13 ili kupata kikosi bora kitakachoshiriki mashindano ya vijana ya mwaka 2021.

No comments:
Post a Comment