Na Zainab Nyamka, Dar
SHIRIKISHO la mpira wa Miguu Nchini (TFF) limesema linatambua uhalali wa
uongozi wa sasa wa timu ya Stand United ambao viongozi wake wamepatikana
hivi karibuni baada ya kufanyika kwa uchaguzi ambao awali ulizua utata na
kuleta sintofahamu kwa wanachama wake na kufikia hatua ya kusimamishwa chaguzi hizo mbili kati ya Stand United wanaojiita wanachama halali na wa
kampuni.
Akitolea ufafanuzi suala hilo, Afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema
kuwa uhalali wa uongozi huo umekubaliwa na kamati ya uchaguzi ya TFF
iliyokutana Julai 13 na kusema kuwa uongozi huo unatambulika kihalali baada ya
kujiridhisha na jina la usajili la klabu hiyo iliyosajiliwa kwa jina la Stand
United Football Club.
"Uchaguzi uliofanyika ni wa haki na TFF tunatambua uhalali wa
uongozi uliopo madarakani kwa sasa", amesema Alfred. Pia uongozi huo wa
Stand unatambuliwa mara baada ya kufanya marekebisho ya daftari lake la
wanachama kama walivyoagizwa na TFF.
Amesema kwa wale ambao hawakushiriki uchaguzi huo (Stand kampuni)
watabaki kuwa wanachama halali wa klabu hiyo hasa wale ambao walienda upande wa
kampuni.
Maamuzi hayo yametolewa na Kamati ya uchaguzi wa TFF walipokutana na
kuangalia kanuni na katiba na kufikia muafaka wa kuuhalalalisha uchaguzi huo
pamoja na Stand United Fc Wakiwa chini ya Makamu Mwenyekiti Domina Madeali.

No comments:
Post a Comment