Na Zainab Nyamka, Dar
MISS Dar Indian Ocean 2016 wamekabidhiwa gari na kampuni ya Helmic Group
Company Limited ikiwa ni maandalizi kuelekea shindano hilo linalotarajiwa
kufanyika hivi karibuni.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi gari hilo aina ya Coaster litakalokuwa
linatumika kwa ajili ya kuwapeleka warembo hao sehemu mbalimbali, Msemaji na
mratibu wa warembo hao Sarah Martin ameshukuru kwa hatua hiyo kutoka
Helmic na kusema kuwa hiyo ni hatua
nzuri kwao kwani kwa warembo waliopo wana uhakika wa kulibakiza taji la Miss
Tanzania kutoka Miss Dar Indian Ocean.
"Kutoka Miss Dar Indian Ocean
tumeweza kutoa warembo mbalimbali na waliweza kuwa Miss Tanzania na hilo
tunajivunia sana kwani ukiangalia Nancy Sumari, Wema Sepetu, Richa Adhia na
Faraja Kota wote walitokea hapa,".
Aidha alisema kuwa, moja ya malengo yao makubwa ni kuweza kuwasaidia warembo wao kufika mbali
hususani kwenye masuala ya urembo.
''Ukizingatia tuna kampuni inayojihusisha na
mitindo basi hatutaweza kuona wanaishia hapa na kupotea zaidi tutawachukua na
kufanya nao kazi zaidi ya hapa.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampini ya Helmic Group Harprit Kaur Sohal alisema
kuwa huu ni mwanzo ila malengo yao makubwa ni kuwasaidia warembo hao katika
shindano lao Miss la Dar Indian Ocean na zaidi wamewapatia gari hilo kwa ajili ya
kuwarahisishia kwenye shindano lao na amewataka warembo kujiamini zaidi.
Mshiriki wa Dar Indian Ocean, Neema Steven Dismas amesema kuwa
akifanikiwa kushinda taji hilo ana imani atazidi kuiwakilisha nchi yetu vizuri
hasa akiweza kwenda kwenye mashindano ya kimataifa kwa kutumia nembo ya Taifa
ambayo ni Mlima Kilimanjaro, Mbuga za wanyama na lugha adhimu ya kiswahili.


No comments:
Post a Comment