Habari za Punde

*YANGA VS MEDEAMA, MAKOCHA WATUNISHIANA MISULI, KAMANDA SIRO AAHIDI USALAMA KUBORESHWA ZAIDI

Na Zainab Nyamka, Dar
MABINGWA wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara na wawakilishipekee wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika Mashariki na Kati, timu ya Yanga imesema kuwa  inahitaji ushindi kwenye mchezo wa kesho na zaidi kocha mkuu wa Yanga Hans Van de Pluijm amesema lazima timu yake itaibuka na ushindi katika mchezo huo ambao ni muhimu kwao.
Amesema, mchezo huo ni muhimu kwao na watahakikisha hawapotezi pointi tatu kwa namna yoyote dhidi ya Medeama mchezo utakaoamua Yanga kusonga mbele au laa.
Katika kuelekea mchezo huo muhimu kwao amewapa wachezaji wake mbinu za jinsi ya kushambulia ili kuhakikisha hawapotezi nafasi wanazozitengeneza. "Katika mchezo uliopita wachezaji wangu walitengeneza nafasi nyingi lakini walishindwa kuzitumia ipasavyo na kufanya tupoteze mchezo wetu wa nyumbani", alisema Pluijm.
Kwa upande wake kocha wa Medeama ya Ghana, Prince Yaw Owusu, ametamba kuibuka na ushindi katika mchezo huo wa kesho dhidi ya wapinzani wake. 
''Nawajua vizuri wapinzani wangu hivyo sina hata wasiwasi na mchezo huo na unasilimia kubwa ya kuondoka na alama tatu. 
"Nina uzoefu na timu ya Yanga kwani nilishaiona katika michuano ya Kagame nilipokuwa na kikosi cha timu ya Al Khartoum ndio maana nasema nina uhakika wa kushinda mchezo wa kesho", alisema.
Nao shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) limewataka Mashabiki na wapenzi wa Yanga kuwa watulivu katika mchezo huo. Ni imani yao kama shirikisho kuwa watashangilia timu yao kwa utulivu na amani ili kuhakikisha inapata alama tatu.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro amesema kuwa ulinzi utaimarishwa katiika mchezo huo ili kuwa na mvuto.
Wananchi wasiwe na shaka yoyote kwani wamejipanga kuhakikisha usalama unasimamiwa kwa asilimia mia na hawatafumbia macho kitendo chochote cha uvunjifu wa amani.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.