Katika mkataba huo kila timu itavuka milioni 42 kwenye kila robo ya msimu
na kwenye robo ya mwisho ambapo kila timu itapata fedha kulingana na nafasi
yake kwenye msimamo wa ligi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi mtendaji wa Azam
Media, Tido Mhando, amesema kuwa mkataba huo umeboreshwa na kila timu sasa
inatakiwa ifanye vizuri ili mwisho wa msimu iweze kupata fedha nyingi zaidi.
Katika msimu huu kumefanyika marekebisho mapungufu yote yaliyojitokeza
katika mkataba uliopita na hata kwenye baadhi ya mechi mliona kulikuwa na
changamoto mbalimbali na tupo kwenye hatua za .mwisho kuzirekebisha.
"Pia kumekuwa na changamoto nyingi sana zilizojitokeza
kipindi cha mkataba wetu wa awali lakini tumezifanyia kazi na kwa sasa zipo
kwenye hatua za mwisho za kuzimalizia ikiwemo vifaa na hata majukwaa ambayo
yatakayokuwa yanatumika kwa ajili ya kuwekea camera kwani viwanja vingi sio
rafiki kwa kazi yetu, "alisema Mhando.
Kwa upande wa TFF, Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi Boniface
Wambura alisema kuwa hii ni hatua nzuri kwao pia na hata kwa vilabu kwani mkataba
umeboreshwa ambapo katika Msimu ujao timu zote zitafaidika sana. Mkataba huu wa
miaka mitano kwa mwaka kila timu itachukua zaidi ya milioni 120.

No comments:
Post a Comment