KATIKA Viwango vya Soka vya FIFA, Tanzania imepanda 13 kutoka nafasi ya 136 hadi 123.
Argentina imeendelea kushikilia nafasi ya kwanza kidunia katika Viwango vya Soka, ikifuatiwa na Colombia huku timu za bara la America ya Kusni zikiendelea kutesa kwa kuingiza timu nne kwenye tano bora na timu kutoka bara la ulaya wakiingiza timu moja ya ujerumani.
Mabingwa wa Ulaya, Ureno wameshika nafasi ya sita huku Brazil wakishuka hadi nafasi ya tisa, Uingereza wameporomoka mpaka nafasi ya 13 na Wales wakipanda kutoka nafasi ya 15 hadi 11.
Bara la Afrika limeonekana kupotea hasa baada ya kushindwa kuingiza hata timu moja kwenye 20 bora na Algeria wakishika nafasi ya 32 huku Ivory Coast wakichukua nafasi ya 35.

No comments:
Post a Comment