Habari za Punde

*WADAU WATAKA MABORESHO YA UTOAJI WA TUZO ZA VODACOM


Na Zainab Nyamka, Dar
WADAU wa michezo nchini wametoa ushari kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF kuboresha zaidi tuzo za Ligi kuu ya Tanzania Bara na kuacha kutumia njia za ujanja katika kuwapata wachezaji wanaostahili kuwania tuzo hizo na kuwapa nafasi wananchi kutumia nafasi yao kuchagua mchezaji aliyeisaidia na kutoa mchango mkubwa kwa timu yake.
Wakizungumza na mtandao huu kwa nyakati tofauti,  Wadau hao walisema kuwa tuzo hizo hazikuwa katika utaratibu mzuri, na hasa katika utaratibu wa kuwapata washindi na jinsi ya kuwapigia kura.
''Tunachojua ni kuwa  waliwataja wanaowania tuzo hizo ila jinsi ya kumpata mshindi ndiyo hatujui wanatumia vigezo gani kumpata mshindi,
"Tunajua wanapiga hatua kwenye utoaji wa tuzo hizo ila changamoto kubwa bado ipo katika upatikanaji wa wachezaji wanaowania tuzo hizo na jinsi gani wanawapata mpaka kuwatangaza na baada ya kuwataja wanatumia njia ipi kuweza kumpata mshindi na kwanini wasilete kwa wadau na kuwapa fulsa ya kuamua na sio wao tena kukaa na kuamua,"walisema.
Tuzo za Vodacom zilifanyika jana usiku huku Timu ya Yanga wakichukua tuzo tano ikiwemo ya Mchezaji bora wa Ligi, Juma Abdul, Mchezaji bora wa Kigeni na Mchezaji Bora mwenye Nidhamu, Thaban Kamosoku, Mfungaji bora Amisi Tambwe, na Kocha Bora Hans Van De Pluijm.
Mohamed Husein 'Tshabalala' alichukua tuzo ya mchezaji chipukizi akiwabwaga Shiza Kichuya na Farid Mussa, Ibrahim Ajib akichukua tuzo ya goli bora la msimu pamoja na Mtibwa timu yenye nidhamu. Na kwa upande wa mwamuzi bora iliangukia kwa Ngole Mwangole kutoka Mbeya.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.