Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) akisikiliza taarifa ya uwanja alipofanya ziara ya kutembelea uwanja uliyowekewa jiwe la msingi na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliyopo eneo la Mtaa wa Makoko Ndumi ,Kata ya Mnyanjani kwa ajili ya kujenga uwanja wa michezo wa kimataifa kwa kushirikiana na FIFA kutoka kwa Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe.Mustapha Selemani leo Jijini Tanga alipotembelea alipofanya ziara ya kikazi kufuatilia maendeleo ya shughuli za kisekta Mkoani hapo.
Baadhi
ya Viongozi wa Muziki wa Mkoa wa Tanga waliyohudhuria mkutano wa wadau
wa kisekta wa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe.Annastazia Wambura (hayupo pichani) leo jijini Tanga alipofanya ziara ya
kikazi yenye lengo la kujua changamoto zao (wakwanza kushoto) Msanii wa Taarabu
Mkongwe Bi. Mwanahela Binti Salim na (wapili kulia) Msanii wa Dansi.
Msemaji wa Timu ya Coastal Union Bw. Oscar Asenga akieleza sababu za timu kushuka daraja kwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni , Sanaa na Michezo (hayupo pichani) leo jijini Tanga alipofanya ziara ya kikazi iliyolenga kukutana na wadau wa kisekta na kuzungumza nao.
Eneo la linalotarajiwa kujengwa Uwanja wa Michezo wa Kimataifa Mkoani Tanga liliyopo Mtaa wa Makoko Ndumi ,Kata ya Mnyanjani ambalo tayari limekwisha wekewa jiwe la Msingi na uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Taifa (TFF) ambapo ujenzi huo utafanywa kwa kushirikiana na Shirikisho la Mipira wa Miguu Kimataifa (FIFA).
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akisalimiana na aliyekuwa Meya wa Jiji la Tanga ambaye ni Msemaji wa Timu ya African Sports Bw.Salim Kisauji leo Jijini Tanga mara baada ya kumalizika kwa mkutano wadau wa kisekta aliyoufanya kaika ziara yake ya kikazi Mkoani hapo.
*************************************************
Anitha
Jonas- MAELEZO
Watendaji wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri watakiwa
kuanzisha Kamati za Michezo
zitakazofanya kazi kwa ukaribu na Baraza La Michezo Taifa (BMT).
Agizo
hilo limetolewa leo jijini Tanga na Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Mhe.Annastazia Wambura alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo
lakutaka kujua maendeleo ya shughuli za kisekta kwa Wizara zinavyotekelezwa
Mkoani hapo na changamoto zake.
“Kamati
hizi za Michezo zitakapoundwa zitasidia kusimamia uendeshwaji wa Michezo katika
Mkoa pamoja na usimamizi wa Vilabu vya Michezo halikadhalika usimamizi wa vyama
vya Michezo kwa kuhakikisha vinakuwa na Katiba pamoja kuzingatia uendeshaji wa
shughuli zake kwa kupitia Katiba hizo ambazo zitatakiwa kuzingatia muongozo”,alisema
Naibu Waziri Mhe.Wambura.
Pamoja
na hayo Naibu Waziri huyo aliwasisitiza kuwa Watendaji wa Mkoa kufanya mchakato
wa kupata Maafisa Michezo waliyotoka katika vyuo vya Michezo vya Serikali kwa
lengo la Maafisa hao kuwa Walimu wa Michezo katika ngazi zote ambapo watasaidia ukuibua wa vipaji vya wanamichezo kuanzia
ngazi ya Kata mpaka Taifa,na kuongeza kipato kwani michezo ni ajira.
Kwa
upande wa Mshahiki Meya wa Jiji la Tanga
Mhe. Mustapha Selemani alimuomba Mheshimiwa Waziri kusaidia kuharakisha ujenzi
wa uwanja wa Kimataifa wa FIFA ambao tayari umeshawekwa jiwe la msingi na
Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) ambapo ujenzi wa kiwanja hicho unatarajiwa
kufanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Naye
Msemaji wa Timu ya African Sports ambaye alikuwa Meya wa Jiji la Tanga Bw.Salim
Kisauji alisema Timu za mpira wa miguu Tanga zimekuwa na changamoto ya ukosefu
wa fedha za uendeshaji na hicho ndiyo chanzo cha kushuka kwa daraja kwa timu hizo katika ligi za taifa.
Pamoja
na hayo Naibu Waziri Wambura alitoa pongezi
Mwalimuwa Mpira wa Basketi Bw. Hemed Rajabu kwa jitihada walizozifanya
zakuibua vipaji vya vijana na kuwasidia vijana 6 kupata nafasi za kusomeshwa Chuo
Kikuu bure na wengine kupata nafasi ya kusomeshwa hata nje ya nchi bure ikiwemo
nje pamoja na hao waliyoko katika shule
za sekondari.
Hata
hivyo viongozi wa Timu za soka Mkoa wa Tanga wametakiwa kufanya jitihada za
kupata mapato ikiwemo kuanzisha michezo ya bahati na sibu katika michezo yao
kwa lengo la kupata fedha za kujiendesha.
No comments:
Post a Comment