TIMU ya Yanga SC imezidi kupoteza matumaini ya kufanya vizuri na kuendelea kushiriki kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani AFrika baada ya leo tena kukubali kichapo cha mabao 3-1 ugenini dhidi ya Medema katika mchezo wa marudiano uliopigwa kwenye Uwanja wa
Essipong Sports mjini Sekondi-Takoradi, Ghana.
Yanga walianza kukubali bao la mapema lililofungwa na
Daniel Amoah dakika ya saba huku mabao mengine yakifungwa na
Abbas Mohammed aliyefunga mabao mawili katika dakika ya 23 na 37, huku bao la kufutia machozi la Yanga likifungwa na Simon Msuva kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 25.
Ikumbukwe kuwa tangu kuanza kushiriki michuano hiyo timu ya Yanga haijawahi kushinda mchezo hata mmoja, zaidi ya kufungwa na kutoa sare moja na Medeama katika mchezo wa kwanza.
Sifa za pekee zimwendee kipa wa Yanga aliyeweza kupangua penati ya
Malik Akowuah katika dakika ya 10,
iliyowafanya Yanga kurejea mchezoni katika kipindi cha kwanza.
Kwa matokeo hayo ya baada ya mchezo wa leo Yanga sasa imepoteza matumani ya kuendelea na michuano hiyo, ambapo sasa inacheza kukamilisha ratiba.
Mazembe inaendelea kuongoza Kundi A kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na MO Bejaia na Medeama ambazo zote kila moja ina popinti tano, wakati Yanga inaburuza mkia ikiwa na kapointi kamoja tu.
Mazembe watakuwa wenyeji wa Bejaia kesho Lubumbashi wakihitimisha raundi za nne.
KIKOSI CHA YANGA:
Deo Munishi ‘Dida’, Kevin Yondani/Andrew Vincent dk46, M. Twite, O. Joshua, J. Abdul/Amissi Tambwe dk73, N. Haroub, H. Niyonzima/Juma mahadhi dk46, T. Kamusoko, D. Ngoma, S. Msuva na O. Chirwa.
KIKOSI CHA MEDEAMA:
Daniel Yaw Agyei, Paul Aidoo, Samjuel Adade, Moses Amponsah Sarpong, Daniel Amoah, Malik Akowuah, Kwesi Donsu, Enock Atta Agyei, Eric Kwakwa/ Kwame Boahene dk72, Abbas Mohammed/ Bismark Oppong dk53 na Benard Ofori.

No comments:
Post a Comment