Na Ripota wa Sufianimafoto Blog, Dar
BAADA ya Simba kutofanya vizuri katika Ligi msimu uliopita kwa kukubali kunyanyaswa na watani wao wa Jadi katika soka la Bongo, Yanga, hatimaye mtanange wa upinzani na kutambiana baada ya usajili wa kila upande baina watani hao, unatarajiwa kupigwa Oktoba
Mosi, mwaka huu katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar esSalaam, leo Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, alisema kuwa mujibu wa ratiba mpya iliyotolewa na Shirikisho hilo leo mchezo huo utakuwa ni wa raundi ya saba ambao utachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Aidha baada ya kusambaa kwa Ratiba hiyo katika mitandao mbalimbali ya kijamii kabla ya kutolewa rasmi na Shirikisho hilo, Alfred aliikanusha ratiba hiyo na kusema kuwa siyo sahihi na kwamba ilikosewa.
“Kwanza niwajulishe kuwa ratiba ambayo ipo kwenye mitandao mbalimbali
siyo halisi kwani anwani iliyopo juu imekosewa na tarehe 21 inaonyesha Azam FC
watacheza wakati siku hiyo kwenye uwanja huo kutakuwe na mchezo wa Serengeti
boys”, alisema Lucas.
Pia Lucas alisema ratiba ya msimu huu imezingatia mechi za kimataifa za timu
za Taifa na Yanga ambayo inashiriki mashindano ya kombe la Shirikisho barani
Afrika hivyo haitakuwa na marekebisho na panguapangua za mara kwa mara kama ilivyokuwa msimu uliopita.
Ratiba ya ligi kuu msimu huu inatarajia kuanza Agosti 20 kwa mechi saba
kuchezwa kwenye viwanja tofauti, lakini mchezo wa Yanga na JKT Ruvu utachezwa
Agosti 31 kutokana na Yanga kujiandaa na mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi
ya TP Mazembe utakaochgezwa Agosti 23.
Kagera Sugar watacheza na Mbeya City Uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera, Simba
wataikaribisha Ndandsa FC, Uwanja wa Taifa, Toto African watakwaana na Mwadui uwanja wa CCM Kirumba.
Michezo mingine Stand United dhidi ya Mbao FC, Mtibwa Sugar
itawakaribisha Ruvu Shooting, Azam FC wataikaribisha African Lyon Uwanja wa Azam
Complex na Majimaji wataikaribisha Tanzania Prison Uwanja wa Majimaji Songea,
Ruvuma

No comments:
Post a Comment