TIMU ya Yanga leo imeshindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Medeama Sc katika mchezo uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya pili ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji wake wa Kimataifa Mzimbabwe, Donald Ngoma, aliyeunganisha pasi nzuri ya Thaban Kamusoko.
Medeama walipata bao la kusawazisha katika dakika ya 17 kipindi cha kwanza kupitia kwa Daniel Amoah, mabao yaliyodumu hadi kumalizika kwa mchezo huo.
Kikosi cha Medeama
Mashabiki wa Yanga ambao haikuweza kufahamika mara moja chanzo cha ugomvi wao wakikunjana na kupigana vichwa wakati mchezo huo ukiendelea.
Ndundi zikiendelea....
Ndundi zikiendelea huku baadhi ya mashabiki wakiamulia ugomvi huo. KWA MATUKIO YA PICHA ZA MTANANGE HUU, NA HABARI KAMILI KAA NASI HAPO BAADAYE.





No comments:
Post a Comment