Habari za Punde

*FULL MKANDA MTANANGE WA YANGA IKILAZIMISHWA SARE NA MEDEAMA, LEO TAIFA

 Mshambuliaji wa anga Donald Ngoma (wa pili kushoto) akiwani mpira na Kipa wa Medeama Sc, wakati wa mchezo waaaao wa Kombe la Shirikisho uliochezwa kweanye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
********************************
 Ripota wa Sufianimafoto,Dar
Na MABINGWA wa Tanzania Bara Dar Young Africans ya jijini Dar es Salaam, leo wameshindwa kutumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kukubali kulazimishwa sare ya 1-1 na wapinzani wao timu ya Medeama ya Ghana katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Kundi A Kombe la Shirikisho.
 Obrey Chirwa wa Yanga, akiwatoka mabeki wa Medeama
*********************************************
Yanga wanaendelea kuburuza mkia katika msimamo wa michuano hiyo baada ya matokeo ya mchezo huo wa leo kwa kujiokotea pointi moja huku wapinzani wao hao Medeama wakiendelea kuwa juu yao katika nafasi ya Tatu katika Kundi A wakiwa na Pointi mbili, Mo Bajaia wakiwa nafasi ya pili na pointi zao Nne huku Kundi hilo likiongozwa na Tp mazembe wenye jumla ya Pointi Sita.
Katika michezo iliyopita Yanga walikubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Mo Bajaia walipokuwa ugenini Algeria na 1-0 wakifungwa tena na TP Mazembe ya DRC katika mchezo uliopigwa nyumbani jijini Dar es Salaam. 
 Kiungo wa Yanga,Mbuyu Twite, akiambaa na mpira baada ya kukwepa kwanja la beki wa Medeama.
************************************************
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Ibrahim Nour El Din, aliyesaidiwa na washika vibendera Ayman Degaish na Samir Gamal Saad wote wa Misri, hadi mapumziko tayari timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1.
Yanga walitangulia kupata kupitia mshambuliaji wake wa Kimataia kutoka Zimbabwe, Donald Ngoma, katika dakika ya pili, akimalizia pasi ya Thabani Kamusoko na kumchambua kipa Daniel Adjei.
 Sehemu ya mashabiki wa Yanga

Baada ya bao hilo, Yanga walisukuma mashambulizi zaidi langoni mwa Medeama, lakini hawakubahatika kuongeza bao.

Medeama wakafanikiwa kuiteka safu ya kiungo na kuanza kutawala mchezo, hatimaye kupata bao la kusawazisha dakika ya 17, lililofungwa na Bernard Donso akimalizia kona ya Enock Atta Adjei baada ya kutokea piga nikupige langoni kwa Yanga, huku mabeki wakionekana kuchelewa kuuondoa mpira huo eneo la hatari.

 Ngoma katikati ya Msitu wa mabeki
******************************************************
Kipindi cha pili, Medeama walikianza vizuri na kuendelea kutawala mchezo, lakini safu ya ulinzi ya Yanga iliyoongozwa na Nahodha Vincent Bossou ilisimama imara.

Mashambulizi ya Yanga hayakuwa ya kushitua langoni mwa Medeama na mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe alionekana kabisa kujilazimisha kucheza akitoka kuugua Malaria.
Almanusra Medeama wapate bao la ushindi dakika ya 90 na ushei baada ya shambulizi la kushitukiza wakitoka kushambuliwa baada ya Abbas Mohamed kupiga mpira uliookolewa na Nahodha Vincent Bossou ukiwa unaelekea nyavuni.


KIKOSI CHA YANGA SC: 
Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua/Juma Mahadhi, Kelvin Yondani, Mtogo Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Obrey Chirwa, Amissi Tambwe/Haruna Niyonzima dk na Donald Ngoma.

KIKOSI CHA MEDEAMAFC; 
Daniel Adjei, Samuel Adade, Moses Sapong, Paul Adoo/Salufu Moro dk62, Daniel Amouah, Kwesi Donsu, Erick Kwakwa, Kwame Boahene, Abbas Mohamed, Bernard Ofori na Enock Atta Agyei/Malik Akowuah dk79. 
 Hapa ni mshike mshike tu....
 Beki wa Yanga, Kelvin Yondani, akiwatoka mabeki wa Medeama
 Ngoma akishangilia bao lake.
 Medeama wakishangilia bao la kusawazisha.....
 Msemaji wa Yanga, Jerry Muro, akiwa jukwaani na mashabiki wa Yanga huku akijichanganaya nao katika harakati za kuishangilia timu yao
 Mashabiki wakishangilia baada ya Yanga kupata bao la kungoza.
 Jerry Muro, akishangilia Jukwaani
 Donald Ngoma,akibinjuka katikati kupiga mpira wa juu ambapo alikosa bao hilo
 Simon Msuva, akitunishiana kifua na kipa wa Medeama, baada ya Msuva kuingia langoni mwa Medeama na kutoa kifuko hicho kilichowekwa na Kipa wa Medeama ndani ya nyavu.
 Donald Ngoma akichuana kuwania mpira na beki wa Medeama.
 Waziri Mahadhi, akiwalamba chenga mabeki wa Medeama na kuachia shuti lililookolewa na kipa wa Medeama.
 Obrey Chirwa akijaribu kumtoka beki wa medeama.
 Mshemaji wa Yanga Jerry Muro, akiongozana na baadhi ya mashabiki wa Simba wakati akiingia uwanjani leo kushuhudia mtanange huo.
Utadhani waelekea Jukwaa moja kumbe waligawanyika hapo hapo chini

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.