Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Maendeleo la Marekani, USAID, Bi. Sharon Cromer, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile, wakitia saini Hati ya makubaliano ya msaada wa Zaidi ya shilingi Bilioni 895, kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka wa fedha 2016/2020, Jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Maendeleo la Marekani, USAID, Bi. Sharon Cromer (Kushoto), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile, wakiwa wameshika Hati za makubaliano baada ya kukamilika kwa tukio la utiwaji saini makubaliano ya msaada wa Zaidi ya shilingi Bilioni 895, kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka wa fedha 2016/2020, Jijini Dar es salaam
Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Mamelta Mutagwaba, wakiteta jambo na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Maendeleo la Marekani, USAID, Bi. Sharon Cromer (Katikati), baada ya kukamilika kwa tukio la utiwaji saini makubaliano ya msaada wa zaidi ya shilingi Bilioni 895, kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka wa fedha 2016/2020, Jijini Dar es salaam.
*********************************************
Na Benny Mwaipaja, MoFP, Dar es salaam
SERIKALI ya Marekani, kupitia shirika lake la Misaada ya Maendeleo
USAID, imeipatia Tanzania msaada wa dola Milioni 407 sawa na zaidi ya shilingi
Bilioni 895 zitakazotumika kwaajili ya kuendeleza sekta za Kilimo, Afya,
Nishati ya Umeme, Elimu na Utawala Bora, katika kipindi cha miaka mitano ijayo
kuanzia mwaka 2016/2020.
Hati za Makubaliano hayo zimetiwa saini Jijini Dar es salaam,
kati ya Mkurugenzi wa Shirika la USAID, Bi. Sharon Cromer, na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha na Mipango Dkt.
Servacius Likwelile.
Msaada huo ni sehemu ya dola Milioni 800, sawa na zaidi ya
shilingi Trilion 1.76 ambazo serikali ya Marekani kupitia USAID, imepanga
kuipatia Tanzania ili kufanikisha Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa katika
kipindi cha miaka mitano ijayo, wenye lengo la kuiwezesha Tanzania kufikia
uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo mwaka 2025.
Kiasi hicho cha fedha kitatumika na serikali ya Tanzania
kupitia mfuko mkuu moja kwa moja wakati kiasi kingine kitatumiwa na Taasisi
zisizokuwa za kiserikali zinazofanya shughuli zake hapa nchini kufanikisha
malengo ya msaada huo.
Miradi iliyopewa kipaumbele ni pamoja na kupambana na UKIMWI
na Kifua Kikuu, Uzazi wa Mpango, Kupunguza vifo vya mama na mtoto, kukuza utawala
wa kidemokrasia, Usimamizi wa Rasilimali za Taifa, na kuwekeza kwenye sekta ya
umeme ili kuimarisha sekta ya viwanda na uzalishaji mali.
No comments:
Post a Comment