Habari za Punde

*SHIRIKA LA HIFADHI YA TAIFA (TANAPA) LAKABIDHI JENGO LA BWALO LA CHAKULA LA SHULE YA SEKONDARI MWIKA

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiq, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi, wakisaini hati ya makabidhiano ya jengo la Bwalo la chakula katika shule ya Sekondari ya Mwika Wilayani Moshi, Jengo hilo limejengwa chini ya ufadhili wa Tanapa kwa kushirkiana na Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mchango wa nguvu za wananchi. Ujenzi huo umegharimu jumla ya Sh. M 186,494,890. 
Baadhi ya Wanafunzi katika shule ya sekondari ya Mwika wakiwa katika hafla fupi ya makabidhiano ya jengo la Bwalo kwa ajili ya Chakula. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akimkabidhi hati, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiq, baada ya kutiliana saini hati ya makabidhiano ya jengo hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadiq akifunua kitambaa kuashiria kuweka jiwe la msingi katika jengo la Bwalo la chakula Shule ya Sekondari Mwika jana. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi.
Baadhi ya Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mwika. 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadiq akizungumza baada ya kuzindua jengo hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza wakati wa hafla hiyo. 
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Betrita Loibooki akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya sekondari ya Mwika lililojengwa kwa msaada wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa ushirikiano na Halmashauri ya wilaya ya Moshi pamoja na wananchi . Picha na 
Dixon Busagaga wa Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.