Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kushoto) akikabidhiwa msaada na Waziri wa Afrika Mashariki Bi. Leontine kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi kwa lengo la kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kushoto) akiongea na wajumbe kutoka
Burundi na Tanzania wakati wa kukabidhi msaada kutoka nchini Burundi kwa lengo
la kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Ujumbe wa Burundi
uliongozwa na Waziri wa Afrika Mashariki Bi. Leontine Nzeyimana (kulia) na Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kushoto (kushoto).
Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akiwakaribisha wajumbe
kutoka Burundi na Tanzania wakati wa mkutano kabla ya kukabidhi msaada kwa
lengo la kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Wa kwanza
kulia ni Waziri wa Afrika Mashariki kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi Bi.
Leontine Nzeyimana na katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba.
Waziri wa Afrika Mashariki kutoka Serikali ya
Jamhuri ya Burundi Bi. Leontine Nzeyimana (katikati) akifafanua jambo na Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kushoto)
mara baada ya kukabidhi ya kukabidhi msaada kutoka nchini Burundi kwa lengo la
kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Kulia ni Mkurugenzi
Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya.
***********************************************************
Burundi
yawafuta machozi Wanakagera kwa tani 183 za vyakula.
Na
Eleuteri Mangi-MAELEZO, Ngara, Kagera.
Serikali
ya Tanzania imepokea msaada wa tani 183 za vyakula mbalimbali kutoka Serikali
ya Burundi kwa ajili ya kuwafuta machozi waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea
mkoni Kagera mapema mwezi huu na kuathiri maisha ya wakazi wa mkoa huo.
Makabidhiano
ya msaada wa vyakula hivyo kutoka nchini Burundi yamefanyika mpakani mwa
Tanzania na Burundi katika eneo la Kituo cha Ushuru cha Pamoja (OSBP) cha Kabanga
wilayani Ngara ambapo Serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba na Mkuu wa
Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu wakati Burundi iliwakilishwa
na Waziri wa Afrika Mashariki Bi. Leontine Nzeyimana na Waziri wa Mambo ya
Ndani wa nchi hiyo Bw. Pascal Barandagiye.
Akikabidhi
vyakula hivyo, Waziri Bi. Leontine amesema kuwa Serikali ya Burundi na Warundi
wote walipatwa na mshtuko mkubwa na majonzi baada kusikia taarifa ya maafa
yaliyowatokea ndugu zao wa mkoani Kagera.
“Kwa
Kirundi tunasema, “Umubanyi niwe muryango” ikimaanisha jirani yako ni ndugu
yako, kwa maana hiyo imekuwa ni wajibu kwa Serikali ya Burundi kuagiza
wawakilishi wake ili waweze kufika hapa nchini Tanzania mkoani Kagera kuwaona
ndugu zetu Watanzania na kuwapa pole”.
Waziri
Bi. Leontine aliendelea kusema “Ndio maana tumekuja na kifurushi kidogo tu ili
tuweze kuwaliwaza ndugu zetu waliofikwa na matatizo hayo” alisema Waziri Bi.
Leontine
Waziri
Bi. Leontine alivitaja vyakula hivyo kuwa ni pamoja na mchele tani 100, mahindi
tani 50, sukari tani 30 na majani ya chai tani 03.
Akizungumzia
suala la mahusiano ya Tanzania na Burundi, Waziri Bi. Leontine amesema kuwa
udugu uliojengeka baina ya nchi hizo mbili na wananchi wake ni wa kihistoria,
si wa leo au wa jana na kusema Serikali yake inadhamira ya kuendeleza udugu huo
vizazi na vizazi huku akiamini Tanzania nayo ina dhamira hiyo hiyo.
Akitoa
shukrani baada ya kupokea msaada huo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba ameishukuru Serikali ya
Burundi kwa msaada waliotoa kwa Tanzania na kuongeza kuwa msaada waliotoa ni
kielelezo cha mahusiano ya karibu na ya kidugu baina ya nchi hizo mbili na watu
wake.
Pia
Naibu Waziri Dkt. Suzan amewataka viongozi wa Serikali ya Burundi wafikishe
salamu na shukrani za dhati za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli kwa Rais wa Jamhuri ya Burundi Pierre Nkurunzinza na
kuwathibitishia kuwa Tanzania itaendeleza uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi
hizo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambao ndio umeathirika na tetemeko hilo Meja
Jenerali Mstaafu Salum Kijuu ambaye pia ni Mkuu wa Ulinzi na Usalama wa mkoa
huo ameihakikishia Serikali ya Burundi kuwa msaada walioutoa utawafikia
walengwa kama ilivyokusudiwa.
Msaada
huo uliotolewa na Burundi umekuwa ni mwendelezo wa misaada inayotolewa na nchi
za Afrika Mashariki kwa Tanzania kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea Septemba
10 mwaka huu na kuathiri mikoa ya kanda ya ziwa.
Burundi
imeungana na nchi za Uganda na Kenya kwa kutoa misaada kwa waathirika wa
tetemeko hilo ambapo September 17 mwaka huu Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipokea
mchango wa fedha taslimu kiasi cha Dola za Kimarekani laki 2 ambazo ni sawa na
takribani Shilingi za Kitanzania milioni 437 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya
Uganda Yoweri Kaguta Museveni na mchango wa mabati, blanketi na magodoro vyenye
thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 115 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya
Kenya Uhuru Kenyatta kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi
Mkoani Kagera.
No comments:
Post a Comment