Msafara wa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, umepata ajali wakati ukiwa safarini kuelekea Wilayani Tandahimba ukitokea Ikulu ndogo ya Rais mkoani Mtwara.
Msafara huo umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa ligula na kuhamishiwa Muhimbili, jinini Dar es Salaam.
Ajali hiyo imetokea mbele kidogo ya kijiji cha Nanguruwe kilichopo Halmashauri ya wilaya ya Mtwara.
Majeruhi walioumia ni dereva pamoja na wasaidizi wanne wa Mh. Makamu wa Rais.
Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa Makamu wa Rais kuacha njia na kupinduka, gari liliokuwa limebeba waandishi wa habari wa channel Ten, Startv na Clouds tv liliacha njia na nusura kupinduka.
Barabara ya kutoka mtwara kuelekea Tandahimba si ya kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi.
Majeruhi wakipatiwa huduma ya kwanza.
No comments:
Post a Comment