Na: Frank Shija, MAELEZO
SERIKALI imewataka walimu wa shule za msingi na
sekondari nchini kuwasilisha madai yao yasiyo kuwa ya Mishahara ikiwemo stahili
za likizo ili waweze kulipwa madai hayo kwa wakati.
Hayo
yamesemwa jana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce
Ndalichako wakati wa mahojiano ya kipindi maalum cha TUNATEKELEZA kinachorushwa
na kituo cha Televisheni cha Taifa (TBC1).
Profesa
Ndalichako alisema kuwa Madeni ya Walimu yamegawanyika katika sehemu mbili
ambazo ni madai yatokanayo na mishahara na yasiyokuwa ya mishahara ambayo
yamekuwa yakilipwa na Serikali kupitia Wizara yake ambapo hadi hivi sasa hakuna
mtumishi ambaye hajalipwa.
“Hakuna
jalada la madai ya walimu yasiyokuwa ya mishahara na kama yapo madai walete ili
walipwe kwani fedha zipo”. Alisema Profesa Ndalichako na kuongeza kuwa madai ya
mishahara yamekuwa yakishughulikiwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma ambapo nayo yamekuwa yakifanyika.
Kwa
mujibu wa Profesa ndalichako alisema Serikali imekuwa ikipata ufadhili kutoka
Serikali ya Sweden kwa ajili ya kusaidia katika kulipa stahili mbalimbali za
walimu ili kuboresha weledi wa taaluma yao.
Kwa
upande wa ubora wa Elimu, Ndalichako alisema kuwa pamoja na changamoto zilizopo
katika sekta elimu, ubora wa Elimu ya Tanzania umekuwa ukifanyiwa kazi kupitia
program mbalimbali zikiwemo za mpango wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).
Akitolea
mfano Waziri Ndalichako alisema kuwa kumekuwapo na maboresho makubwa tokea enzi
za mpango wa UPE miaka ya 1970 ambao lengo lake lilikuwa kuwawezesha wanafunzi
wengi zaidi kujiunga na elimu ya msingi.
Waziri
Ndalichako mwaka 2013 Serikali iliendelea kufanya maboresho kwa kuongeza sifa
za kujiunga na vyuo vya ualimu ili kupata walimu wenye ubora ndipo udahili wa ikiwemo
ufaulu wa daraja la tatu kwa wahitimu wa kidato cha nne na ufaulu wa masomo
mawili katika kidato cha sita.
“Serikali
ilianzisha Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ambayo ilibainisha kuwa elimu
ya msingi na mafunzo mwanafunzi atatakiwa atasoma darasa la kwanza hadi la 6
kwa msingi na mafunzo ni kuanzia darasa la 7 hadi la 12”.

No comments:
Post a Comment