Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki akizungumza na
waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu zoezi la utambuzi na
usajili wa vitambulisho kwa watumishi wa umma litakaloanza tarehe 03 Oktoba.
Kulia kwaker ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Laurian Ndumbaro na Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Seerikali Mtandao (EGA), Dkt. Jabir Bakari.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulkisho vya Taifa (NIDA), Mohammed Khamis Abdallah akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu zoezi la utambuzi na usajili wa vitambulisho kwa watumishi wa umma litakaloanza tarehe 03 Oktoba . Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Seerikali Mtandao (EGA), Dkt. Jabir Bakari. Picha na: Frank Shija, MAELEZO.
********************************************************
Na:
Frank Shija, MAELEZO
SERIKALI inatarajia kufanya
zoezi la utambuzi na usajili wa taarifa za watumishi wa umma kuanzia tarehe 3
Oktoba ili kutoa vitambulisho vya Taifa vilivyo na taarifa zote muhimu za
mtumishi husika.
Hayo yamebainisha na Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah
Kairuki alipokutana na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jijini Dar es
Salaam.
Kairuki amesema kuwa zoezi hilo
la utambuzi na usajili wa wananchi ambalo linaanza na watumishi wa umma ni
muhimu na litasaidia kupunguza gharama kwa Serikali na kuondoa usumbufu kwa
wananchi kwani taarifa zao zote muhimu zitakuwa sehemu moja hivyo kupunguza kero
ya kuulizwa taarifa kila uendapo.
Waziri Kairuki amesema kuwa
zoezi hilo litashirikisha Wizara yake pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa (NIDA), ambapo taarifa zitakazotumika ni zilizilizopo katika vitambulisho
vya mpiga kura.
“Kama mnavyofahamu kuwa
Serikali ipo katika maboresho makubwa ya utendaji wake, hivyo ili kuendana na
hali hiyo tutaanza zoezi la utambuzi na usajili wa watumishi wa umma kuanzia
tarehe 3 Oktoba, zoezi litakalochukua takribani wiki mbili, zoezi hili ni
muendelezo wa Serikali kukabiliana na matatizo ya kutokuwa na taarifa sahihi.”
Alisema Kairuki.
Aidha Kairuki amewata watumishi
wote wa umma kushiriki zaoezi hilo wakiwa na taarifa zote muhimu
zinazowatambulisha ambazo ni pamoja na Cheti cha kuzaliwa, vyeti vya elimu,
kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Mzanzibar Mkazi, hati ya malipo ya
Mshahara, hati ya kusafiria na kadi ya mpiga kura.
Waziri huyo ametoa wito kwa
waajiri kuweka mazingira wezesha ili kufanikisha zoezi hilo ikiwemo kutenga
ofisi itakayotumiwa na kwa kazi hiyo pamoja na kusisitiza waajiri wahakikishe
watumishi wao wanasajiliwa bila kukusa na taarifa ya zoezi hilo iwasilishe
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawabora ndani ya siku 14
tangu zoezi hilo kukamilika kwake.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Laurian
Ndumbaro amewataka watumishi wote wa umma kulipa umuhimu mkubwa zaozi hilo na
kusisitiza kuwa Serikali haita sita kucghukua hatuia za kinidhamu kwa mujibu wa
kanuni za utumishi wa umma kwa mtumishi yeyote atakaye kaidi zoezi hilo.
Awali akijibu swali la
mwandishi wa habari kuhusu namna zoezi hilo litakavyotekelezwa nchi znima kwa
muda wa wiki mbili tu, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA) Mohammed Khamis Abdallah amesema kuwa zoezi hilo litafanikiwa kwani
wanao wafanyakazi zaidi ya 460 nchini nzima ambao wapo katika Ofisi za
Halmashauri.
Pia aligusia suala la vifaa na
kusema kuwa tayari wamewasiliana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo imewapa
mashine za BVR kwa ajili ya kuzitumia katika zoezi hilo la utambuzi na usajili.
Zoezi la utambuzi na usajili wa
wananchi hasa watumishi wa uuma kukabiliana na vyanzo vya watumishi hewa kwa
kuunganisha mifumo ya utambuzi wa watu na mifumo mingine ikiwemo usimamizi wa
rasilimali watu na mishahara katika utumishi wa umma ambapo kuunganishwa kwa
mifumo hiyo kutawezesha mifumo hiyo kuwasiliana na kutumia taarifa zilizo
kwenye kanzi data ya NIDA suala litakalokuwa limerahisisha upatikanaji wa
taarifa.


No comments:
Post a Comment