Katibu
Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Theresia Mmbando akizungumza kuhusu ripoti
ya hali ya maendeleo ya utekelezaji wa
Mpango wa kunusuru kaya maskini(TASAF III) alipokutana na waandishi wa habari
(hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam.
Picha
na: Frank Shija, MAELEZO.
***********************************************************
Na:
Abushehe Nondo & Frank Shija, MAELEZO- Dar
es Salaam.
JUMLA
ya kaya 26,248 zimenufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF III) kwa
kupatiwa jumla ya shilingi Bilioni 6.6 katika mkoa wa Dar es Salaam.
Hayo
yamebainishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando wakati
akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
Mmbando
amesema kuwa utambuzi wa kaya maskini ulianza mwezi Januari 2015 kwa
kushirikisha wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala ambapo jumla ya kaya 26,248 zilizoandikishwa
na kupokea ruzuku kila baada ya miezi
miwili kwa kuzingatia mzunguko wa malipo.
Aliongeza
kuwa wanufaika wa mpango huo wamepatikana kutokana na ushirikishwaji wa jamii
husika ambapo jamii yenyewe ilibainisha majina ya walengwa katika maeneo yao.
Aidha
Mmbando amesema kuwa pamoja na mafanikio hayo kuna baadhi ya changamoto
zilizojitokeza katika kutekeleza mpango huo ikiwemo baadhi ya kaya zilizokidhi
vigezo kukataa kuandikishwa, kuandikishwa kwa kaya zisizokuwa na sifa, pamoja
na kupokea ruzuku pungufu.
Katika
kukabiliana na changamoto hizo, Mmbando amesema mpaka sasa jumla ya kaya 609
zimeondolewa katika kwenye mpango huo ikiwemo kaya 141 (Ilala), kaya 296
(Kinondoni) na kaya 172 (Temeke).
Kwa
upande wake Mratibu wa TASAF Mkoa wa Dar es Salaam, Esterine Sephania amesema
kuwa suala la udanganyifu wa kuandikishwa kwa walengwa wasiokuwa na sifa
linaanzia katika ngazi ya serikali za mitaa ambapo huko ndiko wanaleta majina.
Aliongeza
kuwa kutokana na udanganyifu uliojitokeza katika zoezi hilo takribani shilingi
milioni 2.2 zimepotea kupitia udanganyifu uliotokana na uandikishwaji kwa watu
wasiokuwa na vigezo.

No comments:
Post a Comment