Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii , Eng. Ramo Makani (kushoto) akimkabidhi madawati Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela ( kulia) ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa bungeni mwanzoni mwa mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ya kutengeneza madawati 20,000, wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo Picha na Lusungu Helela- Wizara ya Maliasili na Utalii
Baadhi ya madawati yaliyokabidhiwa jana na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa bungeni mwanzoni mwa mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ya kutengeneza madawati 20,000
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamekaa kwenye madawati mara baada ya makabidhiano yaliyofanyika Mkoani Mwanzan jana na Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongela ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa bungeni mwanzoni mwa mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe .
***************************
Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma
za Misitu Tanzania (TFS) imekabidhi madawati 12,115 mkoani Mwanza ikiwa ni
utekelezaji wa ahadi iliyotolewa bungeni mwanzoni mwa mwaka huu na Waziri wa Maliasili
na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ya kutengeneza madawati 20,000.
Makabidhiano hayo baina ya TFS na Serikali yalifanyika
kitaifa kwenye Uwanja wa chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi.
Naibu wa Waziri wa
Wizara hiyo , Ramo Makani alitoa mwezi mmoja kwa uongozi wa TFS kuhakikisha
unakamilisha kutengenenza madawati 7,885 yaliyosalia kabla ya novemba mwezi huu
‘’ Pamoja na
kufikia asilimia 61 ya lengo, nawaomba TFS muhakikishe idadi iliyobaki ya
madawati inakamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi ujao’’ Alisema Makani.
Akizungumza kabla
ya kukabidhi madawati hayo, Mtendaji Mkuu wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo bila
kutaja gharama iliyotumika alisema ofisi yake imechelewa kufikia asilimia 100
ya kutengeneza madawati 20,000 kutokana na kuwa na changamoto ya ucheleweshwaji
wa taratibu za uvunaji mbao katika baadhi
ya misitu.
TFS tumetekeleza
agizo hili kwa kulenga ngazi za chini kabisa za mfumo wa utendaji wa
Wakala ambao ni wilaya. Hivyo katika
kugawa idadi ya utengenezaji madawati wa kanda ilizingatia idadi ya wilaya kwa
kila kanda’’ alisema Prof. Silayo.
Waziri Makani
alisema madawati hayo yatagawiwa katika mikoa ya Simiyu., Kagera, Mara,Geita na
Mwanza ambayo itapokea madwati 2,580 yaliyokwisha tengenezwa.
Akizungumz kwa
niaba ya Wakuu wa Mikoa ya Tanzania Bara, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela
aliwapongeza TFS na kuahidi kuyatunza madwati hayo ili yatumike kwa muda mrefu
kwa manufaa ya wanafunzi.



No comments:
Post a Comment