Libero wa Timu ya
Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Ally Msengi
(Kulia) akimiliki mpira huku Mshambuliaji wa timu hiyo, Ibrahim Abdallah akipigia
hesabu mpira huo wakati wa mazoezi yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo
wa Jumapili.
Mshauri wa Maendeleo ya soka la Vijana, Kim
Poulsen (kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Msafara wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye
umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Ayoub Nyenzi kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo. Uwanja huo ulioko
kwenye Makutano ya Barabara za Nkolo na Boko, hapa jijini Brazzaville ndio utakaotumika
kwa ajili ya mchezo wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika
kati ya Tanzania na Congo, Jumapili Oktoba 2, 2016.
Huyo ndiye Muhsin
Malima Makame au unaweza ukamwita ‘Super Sub’ wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye
umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, akikokota mpira kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo kuonyesha uwezo
wake uwanjani pindi anapoingia kipindi cha pili kuokoa jahazi. Akikosa kufunga
huwa ni kama bahati mbaya.
Kiungo wa Timu ya
Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Kelvin Nashon
‘akisepa na kijiji cha mabeki’ wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika leo
kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa
Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
Beki wa kushoto wa Timu
ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Nickson
Kibabage akimdhibiti Kelvin Nashon wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika
leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat - Rais wa zamani wa
Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
Baadhi ya viongozi wa Timu
ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, kutoka
kushoto ni Dk. Gilbert Gilbert Kigadye, Mratibu wa timu, Pelegrinus Rutayuga na
Dk. Sheicky Mngazija wakifuatilia mazoezi hayo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse
Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
Kipa Na. 1 wa Timu ya
Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys, Ramadhani
Kabwili akifanya vitu vyake kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse
Massamba-Débat - Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili. Picha na Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, Congo
No comments:
Post a Comment