Pichani Lori kama lionekavyo likiwa nyuma ya basi baada ya kugongana kusababisha mlipuko mkubwa wa moto na kupelekea magari yote mawili kuwaka moto .

Basi la abiria lateketea kwa Moto Kimara Stop Over Jijini Dar leo, mtu mmoja adaiwa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa
Basi lenye namba za usajili T990 AQF mali ya kampuni ya Safari Njema liililokuwa likitokea Dodoma kuja jijini Dar, limeteketea kwa Moto maeneo ya Kimara Stop Over-Suka, mara baada ya kugongana na Lori lililokuwa limebeba shehena ya mifuko ya Cement (namba zake za usajili hazikujulikana mara moja), jioni ya leo, Inaelezwa kuwa mali zote zilikuwemo katika basi vimeteketea kabisa kwa moto.
Jeshi la Polisi limeeleza kuwa mtu mmoja amefariki Dunia katika ajali hiyo na wengine 16 wamejeruhiwa na baadae kukimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu.

Baadhi ya mashuhuda wakishuhudia tukio hilo lilivyokuwa
Gari la zima moto likiwa eneo la tukio kuuzima moto huo.
Baadhi ya Vijana wasio waaminifu walivamia eneo hilo la ajali na kuanza kuondoka na mifuko ya Cement iliyokuwa imebebwa na Lori hilo.
No comments:
Post a Comment