Waziri wa elimu, sayansi Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akiwa na chepe ya mchanga katika ufyatuaji watofali katika Shule ya Sekondari ya Wavulana Nassibugani kabla ya kufunga kambi ya ufyatuaji tofali, Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, (kulia) ni Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega.
******************************************
Na Chalila Kibuda, Mkuranga
Waziri wa elimu, sayansi Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema wananchi wa Mkuranga wamejitoa katika kupata Mandeleo.
Profesa Joyce Ndalichako ameyasema hayo wakati wa kufunga kambi ya kufyatua tofali zaidi ya 45000 kwa ajili ujenzi wa Mabweni Matano na Nyumba tano za walimu katika shule ya sekondari Nassibugani iliyopo kata ya Msonga Wilaya Mkuranga.
Profesa Joyce amesema kuwa wananchi wamejitoa kuhakikisha watoto wanapata elimu bora inayoendana na mazingira.
Amesema kuwa nia yake nikuona Mkuranga inakuwa na Mapinduzi ya Elimu.
Amesema vijana 53 wazalendo kutoka vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi wameamua kuunga mkono jitihada za serikali katika suala la elimu kupewa kiupaumbele katika kusaidia maendeleo ya Taifa.
Amesema ujenzi wa mabweni hayo itakuwa suluhu kwa wavulana kufanya vizuri kutokana kupunguziwa umbali wa kufika shule.
Profesa Ndalichako, amesena jitihada zinaendelea kutatua baadhi ya changamoto za elimu kwa kushirikiana na wananchi.
Katika ufungaji wa kambi hiyo Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amesema nia yake ni kuona maendeleo yanapatikana yenye tija.
Waliohudhuria ufungaji ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, Mkuu wa Wilaya, Filberto Sanga na viongozi mbalimbali.
Waziri wa elimu, sayansi Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akiwa ameshika kibao chenye tofali pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo kabla ya kufunga kambi ya ufyatuaji tofali katika katika shule ya Sekondari Wavulana Nassibugani.

Waziri wa elimu, sayansi Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wazaledo wa vyuo vya ndani na nje ya nchi pamoja na viongozi mbalimbali baada ya kufunga kambi ya ufyatuaji tofali iliyodumu mwezi mmoja.
No comments:
Post a Comment