Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Congo
(DRC) nchini Tanzania Bw. Sumail Edward (kulia) akisisitiza jambo kwa waandishi
wa habari kuhusu uamuzi wa wafanyabiashara wa Congo kutumia Bandari ya Dar es
Salaam baada ya Serikali kuondoa vikwazo, kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara
ya Habari Bw. Tiganya Vincent.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimfuatilia kwa makini Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Congo (DRC) nchini Tanzania Bw. Sumail Edward (mwenye suti) wakati alipokuwa akielezea kuridhika na uamuzi wa Serikali ya Tanzania kuondoa vikwazo katika Bandari ya Dar es Salaam na kupelekea wafanyabiashara wa Congo (DRC) kuendelea kuitumia bandari hiyo.
Picha na Eliphace Marwa - Maelezo
******************************************
Na:
Frank Shija, MAELEZO.
WAFANYABIASHARA
kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wafurahishwa na hatua zilizochukuliwa
na Serikali ya Tanzania katika kuondoa vikwazo vya usafirishaji wa mizigo
kupitia Bandari ya Dar es Salaam.
Hayo
yamebainishwa na Rais wa Wafanyabiashara wa Congo waishio nchini Tanzania Bw.
Sumaili K. Edward alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kurejea
kwao na kutumia Bandari hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Sumaili
amesema kuwa miaka ya nyuma kulikuwa na changamoto nyingi ambapo alizitaja kuwa
ni mizani na sehemu za ukaguzi kuwa nyingi pamoja na siku za kuhifadhi mizigo
kuwa chache.
Alisema
kuwa wamefikia uamuzi wa kuendelea kutumia Bandari ya Dar es Salaam baada ya
Serikali ya Awamu ya Tano kutatua changamo hizo ambapo sasa vizuizi vimepungua.
“Naipongeza
Serikali ya Tanzania kwa hatua ya kutuondolea usumbufu sisi wafanyabiashara wa
Congo tuliokuwa tunafanya shughuli zao Bandari ya Dar es Salaam, tumerejea na
tutapitishia mizigo yetu hapa”. Alisema Sumaili.
Adhai
alisema kuwa wamefarijika kuona sasa siku za kuhifadhi mizigo kabla ya
kuongezeka kutoka siku 15 zilizokuwepo
awali hadi kufikia 30 kama ilivyobainishwa wakati wa ziara ya siku tatu ya Rais
wa Jamhuri wa Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila mapema wiki hii.
Akijibu
swali la la mwandishi wa habari aliyetaka kujua sababu zilizowafanya kusitisha
kwa muda kutumia Bandari ya Dar es Salaam, Rais huyo alisema kuwa kitu kikubwa
kilicho wafanya wachukue uamuzi wa kusitisha ni gharama kuwa kubwa hivyo
kupelekea kufanya biashara isiyokuwa na faida.


No comments:
Post a Comment