Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akipata maelezo kutoka kwa Bw. Leonard Kushoka wa pili kulia katika hatua mbalimbali za uzalishaji wa nishati mbadala.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akiangalia
mkaa uliokamilika baada ya uzalishaji, mkaa ambao ni rafiki kwa
mazingira.
Na Lulu
Mussa, TABORA
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira
Mhe. Jauary Makamba amempongeza Bw. Leordard Kushoka kwa kubuni kiwanda
kinachotengeza nishati mbadala rafiki kwa mazingira.
Akiwa Mkoani
Tabora, Waziri Makamba alipata fursa ya kutembelea kiwanda hicho na kusema kuwa
Serikali inathamini sana ubunifu na uvumbuzi hasa unao okoa mazingira.
"Bwana Kushoka mimi nakupongeza sana, niliona jitihada zako kupitia
kipindi cha televisheni na kuamua kukuita na kukusaidia" alisisitiza
Waziri Makamba.
Katika
kuthamini mchango wa Kiwanda hicho cha "Kuja na Kushoka" Ofisi ya
Makamu wa Rais imemsaidia Bw. Kushoka kupata haki miliki ya Kiwanda hicho.
Awali Bw.
Leonard Kushoka, Mkurugenzi wa Kuja na Kushoka Tools Manufacture Group amesema
kuwa kiwanda chake kimefanikiwa kutoa ajira kwa vijana 13 na kufanikiwa kubuni
teknolojia mbalimbali rafiki kwa mazingira ambapo mpaka sasa wamefanikiwa
kuwafikia vijana zaidi ya 50 katika Wilaya za Tabora Manispaa, Urambo, Kaliua,
Mlele pia Katavi na kufanikiwa kuwafundisha utengenezaji wa Majiko banifu
yanayopunguza matumizi ya kuni na mkaa kwa asilimia 50.
Pia Kiwanda
hicho kimefanikiwa kubuni mashine ambayo ina uwezo mkubwa wa kuzalisha kilo 160
kwa saa kwa kutumia dizeli lita 5 na kuzalisha wastani wa Kilo 1000 za mkaa
mbadala na pia Kiwanda hicho kimefanikiwa kubuni mtambo kwa kukaushia tumbaku
kwa kutumia taka kavu au mabaki yote ya mazao kama maganda ya karanga, randa za
mbao, magunzi ya mahindi na masuke ya mpunga.
Bw. Kushoka
amesema kuwa "Mtambo huu umetoa matokeo mazuri katika ukaushaji wa tumbaku
kwani wastani wa matumizi ya taka kilo 3 hukausha kilo moja ya tumbaku kwa
kutumia mabani ya kisasa"
Bw.
Kushoka amemuomba Waziri kuisaidia Kampuni hiyo kupata mafunzo mbalimbali ya
namna bora zaidi ya kubuni na kuendeleza uzalishaji wa nishati mbadala hasa
katika nchi zinazofanya vizuri zaidi.
'Kuja na
Kushoka" ilianzishwa rasmi mwaka 2000 na kupata usajili mwaka 2013 na
kupewa hati (TMC/CO/CBO/48).
Waziri
Makamba akiwa katika Mkoa wa Tabora pia amepata fursa ya kutembelea Wilaya ya
Nzega na Igunga, akihitimisha ziara yake ya Mikoa 10 hapa nchini yenye
changamoto za kimazingira.
No comments:
Post a Comment