Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na wakuu wa Taasisi na Idara za wizara (hawapo
pichani), wakati wa kikao cha kujadili
masuala mbalimbali ya mipango na maendeleo ya wizara. Kulia ni Naibu Waziri Mhandisi Hamad Masauni. Kikao hicho
kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, jijini Dar es Salaam.
Wakuu wa Taasisi na Idara za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi; Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Wakimbizi pamoja na wakuu wa vitengo wizarani hapo wakimsikiliza Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba, wakati kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya mipango na maendeleo ya wizara. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, akizungumza wakati wa kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya mipango na maendeleo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Idara zake. Kikao hicho kiliongozwa na Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba (hayupo pichani). Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Minja. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, jijini Dar es Salaam .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi



No comments:
Post a Comment