Katibu
Mkuu Kiongozi Mwandishi Balozi John Kijazi (mwenye koti la bluu) akiongoza
matembezi ya hiari ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maadili nchini
yatakayofikia kilele chake tarehe 10 Desemba 2016 katika viwanja vya Mnazi
Mmoja Jijini Dar es Salaam. Matembezi hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam
kuanzia Viwanja vya Karimjee na kuishia Mnazi Mmoja.
Katibu
Mkuu Kiongozi Mwandishi Balozi John Kijazi (mwenye koti la bluu) akiongoza
matembezi ya hiari ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maadili nchini
yatakayofikia kilele chake tarehe 10 Desemba 2016 katika viwanja vya Mnazi
Mmoja Jijini Dar es Salaam. Matembezi hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam
kuanzia Viwanja vya Karimjee na kuishia Mnazi Mmoja. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Katibu Mkuu Kiongozi Mwandishi Balozi
John Kijazi (mwenye koti la bluu) akishiriki katika mazoezi ya viungo baada ya
kumaliza matembezi ya hiari ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maadili
nchini yatakayofikia kilele chake tarehe 10 Desemba 2016 katika viwanja vya
Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Mwandishi Balozi John Kijazi akihutubia washiriki wa matembezi ya hiari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza matembezi hayo leo Jijini Dar es Salaam. Matenbezi hayo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maadili nchini yatakayofikia kilele chake tarehe 10 Desemba 2016 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali Profesa Mussa Assad akizungumza mbele ya mgeni rasmi Balozi John
Kijazi (hayupo pichani) mara baada ya kumaliza matembezi ya hiari leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu
Mkuu Ikulu Peter Ilomo. Matenbezi hayo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya
Maadili nchini yatakayofikia kilele chake tarehe 10 Desemba 2016 katika viwanja
vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, Bw. Valentino Mlowola akifafanua jambo wakati mara baada ya kumalizika kwa matembezi ya hiari leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Mwandishi Balozi John Kijazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa Mussa Assad. Matenbezi hayo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maadili nchini yatakayofikia kilele chake tarehe 10 Desemba 2016 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamishna wa Maadili Bw. Waziri
Kipacha akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Balozi John Kijazi mara baadaa
ya kuhitimisha matembezi ya hiari leo Jijini Dar es Salaam. Matenbezi hayo ni sehemu ya maadhimisho
ya Siku ya Maadili nchini yatakayofikia kilele chake tarehe 10 Desemba 2016
katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Mwandishi Balozi John Kijazi (mwenye koti la bluu) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na watumishi kutoka Taasisi zinazosimamia maadili, uwajibikaji, Utawala Bora, haki za binadamu na mapambano dhidi ya rushwa.mara baada ya kumaliza matembezi ya hiari ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maadili nchini yatakayofikia kilele chake tarehe 10 Desemba 2016 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Kiongozi Mwandishi Balozi John Kijazi (mwenye koti la bluu) akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya viongozi kutoka Taasisi zinazosimamia maadili,
uwajibikaji, Utawala Bora, haki za binadamu na mapambano dhidi ya rushwa pamoja
na watoto mara baada ya kumaliza matembezi ya hiari ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya Siku ya Maadili nchini yatakayofikia kilele chake tarehe 10
Desemba 2016 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Picha
zote na: Ally Mataula – Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
************************************************************************
Na
Joseph Ishengoma
Serikali
imesema kuwa imedhamiria kwa dhati kupambana na rushwa za kila aina ili kujenga
jamii yenye maadili na inayochukia vitendo vya rushwa.
Katibu
Mkuu Kiongozi Mhe. Mwandisi Balozi John Kijazi amesema hayo leo jijini Dar es
Salaam wakati akihitimisha matembezi ya watumishi wa taasisi zinazosimamia
maadili, uwajibikaji, utawala bora, haki za binadamu na mapambano dhidi ya
rushwa.
Matembezi
hayo yameanzia katika viwanja vya Karimjee hadi Mnazi Mmoja na kuzishirikisha taaasisi zinazohusika na
masuala ya utawala bora.
Taasisi
hizo ni Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, taasisi ya kuzuia na
kupambana na rushwa, mamlaka ya kudhibiti manunuzi ya umma, na ofisi ya Taifa
ya ukaguzi wa hesabu.
Taasisi
nyingine ni Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Tume ya Utumishi wa Umma,
na Tume ya Haki za Binadamu.
“Ipo
mifano ya sehemu ambazo rushwa imekithiri kutokana na vitendoi vya rushwa na
ufisadi. Kiongozi mkubwa anashindwa kumsimamia mtu aliyechini yake kama sheria
ya maadili inavyomtaka kwasababu yeye mwenyewe mikono yake si misafi,” amesema
na kuongeza kuwa , “matokeo yake hata mtu awe na mali nyingi, bado ataendelea
kula rushwa bila kikomo”.
Balozi
Kijazi amesema, “serikli ya awamu ya tano imedhamiria kupambana na rushwa ya
aina zote kwa lengo la kujenga jamii yenye maadili inayochukia vitendo vya
rushwa na ufisadi.”
Kwa
mujibu wa Balozi Kijazi, jitihada za
serikali ni kuondokana na hulka ya ubinafsi na uroho na kujenga utamaduni na
tabia ya kijitolea.”
Aidha
Katibu Mkuu Kiongozi ametoa wito kwa waandishi wa habari na vyombo vya habari
kuonyesha uzalendo kwa kuielimisha jamii kuhusu maswala ya maadili nchini.
“Natoa
wito kwa waandishi wa habari na vyombo vya habari kuonyesha uzalendo kwa taifa
letu kwa kuielimisha jamii kuhusu kujenga, na kukuza maadili, haki za binadamu,
uwajibikaji, utawala bola na mapambano dhidi ya rushwa,” amesema.
Awali
akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino
Mlowola ameeleza kuwa lengo la matembezi hayo ni kutuma ujumbe kwa wananchi
kuhusu kujenga na kukuza maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora
na mapambano dhidi ya rushwa.
Kamishna
Mlowola amesema, kuanzia Jumatatu ijayo, taasisi zinazohusika na masuala ya
utawala bora zitakuwa na wiki ya utoaji huduma katika viwanja vya Mnazi Mmoja
ili kupokea kero na malalamiko ya wananchi na kisha kuyashughulikia.
“Hii
ni moja ya kampeini ya taasisi husika kuikataa rushwa, kujenga maadili na
misingi ya uadilifu na kuhamasisha jamii kujua haki zao,” amesema.
Kampeini
hii ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu iliyoanza
Novemba 10 mwaka huu ambayo kilele chake ni Desemba 10, 2016.
No comments:
Post a Comment