
Jengo la kisasa la Kitegauchumi la Chama Cha Mapinduzi (CCM), lilipo Upanga jijini Dar es Salaam, lililozinduliwa leo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Abdulrahman Kinana.
Kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa Mali za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Anna Abdallah, ujenzi wa jengo umegharimu sh. Bilioni saba.Mama Anna Abdallah, amesema, jengo hilo limejengwa kwa hali ya juu na limewekwa kila kitu ikiwemo zamani.
"Mpangaji anapotaka kuingia katika nyumba hii, yeye anachopaswa kufanya ni kuja na chakula na nguo tu, halazimiki kuingia na samani yoyote hata TV anaikuta ipo sebuleni", Alisema, Mama Anna.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikata utepe kuzindua rasmi jengo hilo. Kushoto kwake ni Mama Anna Abdallah na kulia kwake ni Mama Zakia Meghji. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Zakia Meghji akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la Kisasa la Kitegauchumi la CCM, lilipo Upanga jijini Dar es Salaam, leo.
Baadhi ya waalikwa wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo la kisasa la kitegauchumi la CCM, Upanga jijini Dar es Salaam, leo.









Samani ndani ya jengo

No comments:
Post a Comment