Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Bunge, Kazi, Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu Mhe.Jenister Mhagama akimskiliza
Rais wa TUCTA Bw. Tumaini Nyamghokya wakati viongozi wapya wa TUCTA
walipomtembelea Ofisini kwake Magogoni Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu Mhe.Jenister Mhagama akizungumza na uongozi mpya wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini(TUCTA) ofisini kwake Magogoni Jijini Dar es Salaam.Waziri uyo amehaidi kuwapa ushirikiano wa kutosha viongozi hao ili kuleta tija na ufanisi katika sekta ya kazi.
************************************************************
Na
Daudi Manongi-MAELEZO
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu,
Jenister Mhagama amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa viongozi
wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) ili kuleta tija na ufanisi
katika sekta ya kazi.
Waziri
Mhagama aliyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wake na
Viongozi hao wa TUCTA waliofika ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha mara
baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa shirikisho hilo.
“Tumefarijika
sana kwa TUCTA kupata uongozi mpya ambao tuna uhakika wanachama wamezingatia masuala muhimu katika uchaguzi wao ikiwemo weledi na kutazama
dira ya sekta ya wafanyakazi nchini”.
Aidha
aliongeza kuwa Viongozi hao wana jukumu kubwa la kuleta tija na maendeleo chanya
katika sekta ya kazi nchini na kuhimiza kuwa wafanyakazi ni rasilimali muhimu katika
kuleta maendeleo ya nchi.
Kwa
mujibu wa Mhagama ameahidi Viongozi hao kufanya kikao kazi mapema iwezekanavyo kwani
uchaguzi umekwisha na sasa kilichobaki ni kufanya kazi.
Pia
amesisitiza ushirikiano wa kudumu kati ya Serikali, Waajiri na wafanyakazi
ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua migogoro iliyopo.
Kwa
upande wake Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamghokya alimshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
kwa kusimamia utu wa mtumishi kwa kuhaidi kuwalinda kutokana na baadhi ya viongozi
kutoa lugha zisizosahihi.
Aidha,
ameishukuru Serikali kwa kuwa karibu nao kwa muda wote na kuhaidi kuendeleza ushirikiano
huo ili kuleta tija katika kazi.
No comments:
Post a Comment