Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Fedha
(TRA) Bi. Anna Mndeme (kulia) akipokea tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu kwa
taasisi za umma kutoka kwa Mwakilishi wa
Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw .Shogolo Msangi katikati wakati wa sherehe za kukabidhi tuzo hizo kwa wawasilishaji bora wa mapato kwa mwaka 2015
yaliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es salaam wa kwana kushoto ni
Mwenyekiti wa NBAA Prof. Isaya Jairo.
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt.Ayoub Rioba kulia akipokea tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu kwa taasisi za umma baada kuwa mshindi wa pili kutoka kwa kwa Mwakilishi wa Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw .Shogolo Msangi kushoto wakati wa sherehe za kukabidhi tuzo hizo kwa wawasilishaji bora wa mapato kwa mwaka 2015 yaliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Afisa Mkuu wa Mapato kutoka kampuni ya
kutengeneza sementi (Tanga Cement Plc) Bw. Pieter De Jager wa pili kulia akiwa
ameshika tuzo ya washindi wa jumla kwenye masindano ya wawasilishaji bora wa
mapato kwa mwaka 2015 yaliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Mwakilishi wa Mhasibu Mkuu wa
Serikali Bw. Shogolo
Msangi (katikakati waliokaa) akiwa katika
picha ya pamoja na washindi wa uwasilishaji bora wa mapato wakati wa sherehe za kukabidhi tuzo hizo kwa
mwaka 2015 iliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Picha Na Ally Daud-Maelezo
***********************************************************
Na
Ally Daud-MAELEZO
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA)
imeshinda tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu kwa taasisi za umma zilizoandaliwa na Bodi ya Ukaguzi na Wahasibu (NBAA) kwa mwaka
2015.
Akipokea tuzo hiyo Naibu Mkurugenzi wa
Idara ya Fedha (TRA) Bi. Anna Mndeme amesema kuwa wamepata tuzo hiyo kutokana
na kuwasilisha vizuri mahesabu ya mwaka
wa fedha yaliyowasilishwa kufuatana na viwango vya uwasilishwaji vinavyozingatiwa na Bodi ya Ukaguzi na
Wahasibu (NBAA).
“Tumefanya vizuri na tumepata tuzo kwa
kushika nafasi ya kwanza kutokana na
kuwasilisha vizuri mahesabu ya mwaka wa fedha yaliyowasilishwa kufuatana
na viwango vya uwasilishwaji
vinavyozingatiwa na Bodi ya Ukaguzi na Wahasibu (NBAA)” alisema Bi.
Mndeme.
Aidha Bi. Mndeme amesema kuwa tuzo
hiyo ni chachu kwa TRA itayofanya waendelee kujituma zaidi katika ukusanyaji na
utunzaji wa mapato ili kusaidia nchi kupata huduma bora za jamii kwa maendeleo
ya taifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma
na Elimu kwa Mlipakodi TRA Bw. Richard Kayombo amesema kuwa huo ni uthibitisho
kwamba TRA inafanya kazi kwa ueledi na
uwazi kupelekea kupata tuzo ya heshima.
Katika mashindano hayo Shirika la
Utangazaji la Taifa (TBC) wameibuka washindi wa pili huku kampuni
inayotengeneza Sementi (Tanga Cement
Plc) wakiibuka kuwa washindi wa jumla kwenye tuzo hizo .
No comments:
Post a Comment