Afisa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka TRA Idara ya Kodi za Ndani Bw. George Haule akitoa mada wakati wa semina ya wajasiriamali wanawake iliyofanyika wakati wa maonesho ya viwanda vya Tanzania jana jijini Dar es Salaam.
*********************************************************
Na
Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa mafunzo kwa wajasiriamali kuhusu kodi ili waweze
kufahamu aina na madaraja ya kodi pamoja na umuhimu wa ulipaji kodi.
Mafunzo
hayo yametolewa jana na Afisa wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, George
Haule katika semina ya wakina mama wajasiriamali iliyoandaliwa na Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) na kufanyika katika viwanja vya
Sabasaba vilivyopo jijini humo.
Haule
amesema kuwa katika uanzishaji wa biashara ya aina yoyote jambo la kwanza na
muhimu ni kujisajili katika mamlaka hiyo na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa
Mlipa Kodi (TIN - Number) itakayomuwezesha mfanyabiashara au mjasiriamali kuwa
na biashara halali ambayo inalipiwa kodi kulingana na mauzo au faida ya
biashara husika.
”Tanzania
ni nchi yetu na sisi Watanzania ndio tuna jukumu la kuitunza nchi hii, njia
rahisi ya kuitunza nchi ni kulipa kodi stahiki ili kuinua pato la taifa kwa
sababu kodi ndio chanzo kikubwa cha mapato ya nchi,”alisema Haule.
Haule
ameongeza kuwa Serikali ya Tanzania inatumia mfumo endelevu wa ulipaji kodi kwa
maana ya kila mfanyabiashara mdogo mwenye mauzo yasiyozidi 20,000,000 kulipa
kodi ya mwaka kulingana na mauzo yake na mwenye mauzo yatakayozidi kiasi hicho
cha fedha kulipa kodi ya mwaka kulingana na faida anayoipata katika biashara
husika.
Amefafanua
kuwa wafanyabiashara wadogo wamegawanyika katika makundi matano ambapo wenye
mauzo ya kuanzia shilingi 1 hadi 4,000,000 kwa mwaka hawalipi kodi yoyote,
wenye mauzo kuanzia 4,000,000 hadi 7,500,000 wanalipa kodi ya shilingi 150,000
kwa mwaka, wenye mauzo kuanzia 7,500,000 hadi 11,050,000 wanalipa shilingi
318,000 kwa mwaka, wenye mauzo kuanzia 11,050,000 hadi 16,000,000 wanalipa
shilingi 546,000 kwa mwaka na wenye mauzo kuanzia 16,000,000 hadi 20,000,000
wanalipa shilingi 862,000.
Ameendelea
kufafanua kuwa mfanyabiashara mwenye mauzo ya zaidi ya 20,000,000 sheria
itamtaka aandae mahesabu ya mauzo yake ili aweze kulipa kodi kulingana na faida
anayoipata kwa mwaka mmoja.
Amewaasa
wafanyabiashara kufuata sheria na taratibu zilizowekwa kwa ajili ya ufanyaji wa
biashara nchini ili kwa pamoja tushirikiane katika kuijenga Tanzania yenye
maendeleo.
No comments:
Post a Comment