Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiongea na wadau mbalimbali katika uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo (jana).
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizindua Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo (jana). KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr. Albina Chuwa akiongea na wadau mbalimbali katika Uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo (jana).
Meneja wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Sylivia Meku akielezea kwa wadau wa afya Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo (jana).
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr. Albina Chuwa kabla ya uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo (jana), katikati ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr. Mohamed Ally
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akiwa katika picha ya pamoja wadau mbalimbali wa Takwimu na Afya katika
uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya
Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo (jana). Picha na Benjamin Sawe- Maelezo
*****************************************
Na. Eliphace Marwa – Maelezo
SERIKALI imezindua ripoti ya utafiti
wa afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya malaria ya mwaka 2015/16 mapema hii
leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni awamu ya tatu katika ugonjwa wa malaria
ambapo ripoti imeonesha kupungua kwa vifo vya watoto wadogo.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mgeni
Rasmi ambaye pia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mh. Ummy Mwalimu ameipongeza Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kuaanda ripoti
iliyoonesha Taifa kupiga hatua katika utoaji wa huduma ya mama na mtoto.
Waziri Ummy ameeleza kuwa ripoti hiyo
itaisaidia Wizara ya Afya na serikali kwa ujumla katika kutathmini na
kufuatilia utekelezaji wa mipango endelevu katika huduma za afya hapa nchini
ili kuboresha utoaji wa huduma ambazo ripoti imeonesha haikufanya vizuri
kutokana na changamoto mbalimbali ambazo ripoti imezibainisha.
“Ripoti hii imeonesha kuwa bado kuna
changamoto katika mimba za utotoni kwani zimeongezeka ukilinganisha na mwaka 2010
ambapo watoto 23 kati ya mia moja walipata mimba wakiwa na umri mdogo
ukilinganisha na sasa watoto 27 kati ya mia moja hupata mimba katika umri mdogo
hivyo kuna haja ya jamii kuelimishwa juu ya madhara ya mimba za utotoni”,
alisema Waziri Ummy.
Aliongeza kuwa kuna haja ya serikali
kuangalia upya sheria ya kuruhusu mwanafunzi kuendelea na masomo endapo akipata
mimba akiwa shuleni kwani kumzuia kuendelea na masomo ni kupoteza nguvu kazi ya
taifa na kuikwamisha serikali kufikia malengo yake ya uchumi wa viwanda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa
Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa amesema kuwa iwapo huduma za afya
zitaboreshwa zitapelekea ukuaji wa uchumi kwasababu ya uwepo wa nguvu kazi ya
uhakika na kuongeza uzalishaji kwa Taifa.
“Wananchi wakiwa hawana afya ya
kutosha na kuugua mara kwa mara uchumi wa nchi yoyote Duniani hupungua kasi ya
ukuaji kwa kuwa rasilimali fedha ambazo zingeelekezwa kukuza sekta nyingine
hupungua na hata nguvu kazi kupungua” alisema Dkt. Chuwa.
Aidha Dkt. Chuwa aliongeza kuwa kwa
mujibu wa Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 inatamka kuwa yeyote atakaepotosha
Takwimu hizi kwa makusudi atachukuliwa
hatua za kisheria kupitia kifungu cha 37
cha sheria hiyo.
Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto wa
mwaka 1991-92 ulionyesha kuwa katika kila watoto 1000 wanaozaliwa hai, watoto
141 walikuwa wakifariki kabla ya kufikia umri wa miaka mitano ila utafiti huu
umebaini kuwa ni watoto 67tu ndiyo wanaofariki kati ya watoto 1000.
No comments:
Post a Comment