Habari za Punde

KILOLO NA MUFINDI KUNUFAIKA NA KILIMOCHA ZAO LA PARETO

 Na Tulinkisa Ndelwa na Hawa Mohamed
WAKULIMA wa wilaya ya Kilolo na Mufindi mkoani Iringa wanatarajia  kunufaika na kilimo cha zao la pareto baada ya kiwanda cha Pyrethrum company Tanzania Ltd (PCT) Mafinga kuanza kugawa bure miche ya zao la Pareto.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa uhamasishaji wa kilimo cha zao la Pareto kata ya Bomalang'ombe na Idete mwakilishi wa kiwanda cha PCT Godfrey Mbeyela, alisema kampuni hiyo imeamua kutoa miche bure ili kuwaondolea usumbufu wananchi wa kupata miche.
"Kwa mwaka huu miche ipo ya kutosha ya kuwawezesha wananchi zaidi ya 40,000 kulima Pareto ila kwa kuwa idadi ya wakulima inaweza ongezeka zaidi mwakani vikundi vitapewa kazi ya kuotesha miche na kuuza kwa kampuni….. kampuni haitaki mkulima wa zao la Pareto kununua miche"alisema Mbeyela

Na kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah aliwataka wananchi kujiunga na kilimo hicho kwani ni moja kati ya mazao ambayo hayahitaji gharama kubwa ya kuhudumia zaidi ya palizi pekee.Hivyo alishauri kila mwananchi kulima japo ekari moja ya Pareto.
Awali wananchi wa Wilaya ya mufindi walisema kuwa waliacha kulima pareto na kufyeka mashamba kisha kupanda viazi baada ya kuyumba kwa soko la Pareto. 
Sehemu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.