Habari za Punde

SIMBA YAPIGWA 'STOP' NA MTIMBWA LEO, YATOA SARE 0-0 UWANJA WA JAMHURI

Henry Joseph wa Mtibwa Sugar,  akimiliki mpira mbele ya Kiungo wa Simba Mwinyi Kazimoto, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jioni ya leo. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 0-0.
***********************************************
Na Zainab Nyamka, Morogoro.
Timu ya Simba leo imeshindwa kuendeleza ushindi na kuondoka na pointi tatu kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro baada ya kulazimishwa sare ya kutokufungana na wakata miwa wa Morogoro mtibwa Sugar.

Baada ya matokeo hayo Simba wanaendelea kusalia kileleni wakiwa na alama 45 juu ya Mtani wake Yanga kwa tofauti ya Pointi 2 wenye Pointi 43 baada ya wao kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi yao ya jana dhidi ya Majimaji Songea.

Baada ya mchezo huo Simba wanatarajia kushuka dimbani Januari 28 kwenye Uwanja wa Uhuru kuvaana na Azam Fc.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.