Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Profesa Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi Mpya
ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –Board) leo Jijini Dar es
Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Peter Maduki na Kaimu
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Dkt. Bwire
Ndazi. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Mamlaka
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo
leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Mamlaka
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo
leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akimpa maelekezo Mwenyekiti Mpya wa Bodi
Mpya ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –Board), Peter Maduki
(kulia) mara baada ya kumkabidhi taarifa ya utekelezaji wa Mamlaka ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo leo
Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akimsikiliza mmoja wa wajumbe wa Bodi ya
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET – Board) kupitia Bakwata
Suleiman Lolila (kulia) mara baada ya kuzindua Bodi hiyo leo Jijini Dar es
Salaam. Katikati ni Mwenyekiti Mpya wa Bodi hiyo Peter Maduki (katikati).
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
wajumbe wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –
Board) wakati wa hafla ya uzinduzi wa
Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Waliokaa kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi
wa VETA Dkt. Bwire Ndazi na Kushoto ni Mwenyekiti Mpya wa Bodi, Peter Maduki.
*****************************************************************
Na:
Frank Shija, MAELEZO.
BODI
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –Board) imeagizwa kuanza mara moja
kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo utekelezaji wake umekuwa ukisuasua kwa
muda mrefu huku kukiwa na fedha zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji miradi
hiyo.
Agizo
hilo limetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na wakati akizindua Bodi Mpya ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET
–Board) leo Jijini Dar es Salaam.
Profesa
Ndalichako ameshangazwa na kitendo hicho cha ucheleweshaji wa utekelezaji wa
miradi hiyo huku kukiwa na shilingi takribani bilioni 14.5 zilizotengwa katika
bajeti ya mwaka wa fedha 2016/207 kwa ajili ya kazi hizo.
“Inasikitisha
kuona kuwa tunakaribia robo ya mwisho ywa mwaka wa fedha 2016/2017, huku karibu
miradi yote ya maendeleo haijaanza kutekelezwa,isipokuwa ile tu ya kujengea
uwezo na siyo ya ujenzi wa VETA ambazo ndiyo hitaji kubwa kwa sasa.”Alisema
Profesa Ndalichako.
Ndalichako
ameongeza kuwa Bodi hiyo inapaswa kuanza kazi mara moja ikiwa ni pamoja na
kuwachukulia hatua watendaji watakao bainiuka kuhusika katika ucheleweshaji wa
kuanza kwa miradi hiyo.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo Peter Maduki amempongeza Waziri Ndalichako
kwa kuwa muwazi katika kuelezea kutolridhishwa na udhaifu katika utendaji kwa
baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka hiyo na kuahidi kushughulikia suala hili huku
akiwataka wajisahihishe badala ya kusubiri kuwajibishwa.
“Mhe
Waziri, maelekezo yako tumeyapokea, nikuahidi tu kuwa mimi pamoja na timu yangu
tutayafanyika kazi, ni nisememe wazi tupo tayari kushirikiana nawe wakati
wowote,” alisema Mduki.
Awali
akisoma maelezo mafupi kuhusu Bodi ya Mamlaka hiyo wakati, Kaimu Mkuu wa
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA) Dkt. Bwire Ndazi amebainisha
changamoto kadhaa katika eneo hili la utoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi
stadi kuwa ni pamoja na uwezo mdogo wa VETA na wadau katika kufikia mahitaji ya
elimu na mafunzo ya ufundi akitolea mfano kuwa watu wanaohitaji kujiunga na
mafunzo wanakadiriwa kuwa laki sita kwa mwaka, uwezo wa vyuo vyote vya VETA,
VYA Serikali na binafsi ni kati ya 125,000 tu kwa mwaka.
Bodi
iliyomaliza muda wake iliundwa Agosti 2011 na kumaliza muda wake kisheria
Agosti 2014, na baadaye kuongezewa muda hadi desemba 2016 alipoteuliwa Mwenyekiti Mpya wa Bodi
hiyo yenye jumla ya wajumbe 10 kutoka maeneo ya ujuzi mbalimbali.






No comments:
Post a Comment