Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe mara baada ya kuweka jiwe la
msingi la kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles)
cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd. kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani
leo.Kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega, Mkuu wa Mkoa wa
Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanzania
Goodwill Ceramic Tiles Ltd Fang Habibi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara
na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru (wapili kulia).
Na Benjamin Sawe, MAELEZO- Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli amezuia usafirishaji wa mchanga wa madini kwenda kuuchenjua nje ya nchi akitaka shughuli hizo zifanyike nchini.
Akizungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengeneza vigae cha Tanzania Goodwill Ceramic Rais, Magufuli alisema uchenjuaji wa mchanga wa madini nje ya nchi kunaikosesha Serikali mapato ikiwa ni pamoja na wizi madini hayo.
”Ndio maana nilikataa kusaini mkataba wa EPA kwa sababu kupitia mkataba huo, ni vigumu kwa kampuni za Tanzania kushinda zabuni katika nchi za Ulaya lakini ni rahisi kwa kampuni za Ulaya kushinda zabuni Tanzania kutokana na kukomaa kiteknolojia, na hata zinaposhindanishwa kampuni za Tanzania na Ulaya ni rahisi kwa kampuni za Ulaya kushinda, jambo litakalochangia kuua kampuni zetu”alisema Rais Magufuli. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Jiwe la msingi la kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd kama linavyooneka mara baada ya baada ya kuwekwa rasmi leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi wa kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles)
cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd mara baada ya kuweka jiwe la msingi leo
Wilayani Mkuranga, Pwani. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani
8000 za Vigae kwa siku.Kushoto kwake ni Balozi wa China nchini Tanznia Dkt.Lu
Youqing na kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na
Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist
Ndikilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd mara baada ya kuweka jiwe la msingi leo Wilayani Mkuranga, Pwani. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 8000 za Vigae kwa siku.Kushoto kwake ni Balozi wa China nchini Tanznia Dkt.Lu Youqing na kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd leo Wilayani Mkuranga, Pwani. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 8000 za Vigae kwa siku.Kushoto kwake ni Balozi wa China nchini Tanznia Dkt.Lu Youqing na kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru (kulia) akimsikiliza kwa makini Naibu Mkurugenzi wa kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd, Robin Huang (kushoto) wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho leo Wilayani, Mkuranga.Katikati ni Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho jina lake (limehifadhiwa).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuwaaga wananchi na wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic
Tiles Ltd kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani mara baada ya kuweka jiwe la msingi
leo wilayani Mkuranga, Pwani.
Baadhi ya wananchi wakitawanyika mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani) kuondoka baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd kilichopo Mkuranga, Pwani. Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.
****************************************************
Alisema
Tanzania ni mwananchama wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi wanachama
wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC hivyo kujengwa kwa kiwanda hicho kutapelekea
kiwanda hicho kunufaika kiuchumi.
Rais Magufuli alisema kwa muda mrefu wawekezaji
wamekuwa wakisafirisha malighafi za Tanzania nje ya nchi kwa ajili ya uzalishaji
na kupelekea wananchi kutumia bidhaa zisizo na ubora.
Katika uwekaji wa jiwe la msingi wa Kiwanda hicho
Mheshimiwa Magufuli alisema imefika wakati kwa Tanzania kuuza bidhaa zinazozalishwa
viwandani na kuachana na kusafirisha malighafi nje ya nchi kwa ajili ya
uzalishaji.
Katika hatua nyingine Rais John Pombe amesema
Serikali yake haina chakula cha kuwapa wananchi wanaopatwa na tatizo la njaa
badala yake amewataka wananchi kufanyakazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na
kuzalisha chakula cha kutosha.
Awali akitoa salamu zake kwa Mheshimiwa Rais,
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Adelhelm Meru amesema kujengwa kwa
kiwanda hicho ni faida kwa uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Nae Balozi wa Tanzania nchini Mhe. Lu Youqing alisema Serikali
ya China kwa sasa iko katika mkakati wa kuhamishia viwanda vyake vingi barani
Afrika na imeamua kuichagua Tanzania kuwa moja kati ya nchi watakazohamishia
viwanda hivyo kutokana na kuridhishwa na dhamira inayoonyeshwa na serikali
katika kuleta maendeleo.
Alisema
China inatambua mchango mkubwa wa Tanzania katika harakati za kujikomboa hivyo
itaendelea kuiunga mkono kuhakikisha inafikia uchumi mzuri.









No comments:
Post a Comment