Kaimu Mkurugenzi kutoka Kamisheni ya Usuluhishi na Uamuzis(CMA)Bw. Shanes Nungu (kushoto aliyevaa suti nyeusi) na Afisa Mgavi Mkuu, Bw. Raphael Towo kutoka CMA wakisaini Mkataba wa Makubaliano ya Viwango vya Huduma Baina ya Mahakama na Kamisheni ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).
Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ilvin Mugeta (kulia) akisaini Mkataba wa Makubaliano ya Viwango vya Huduma Baina ya Mahakama na Kamisheni ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), huku akishuhudiwa na Mtendaji anayeshughulikia Mahakama Kuu, Mhe. Samson Mashalla(kushoto). Mkataba huo una lengo la kuhakikisha kwamba Mahakama ya Tanzania na Wadau wa nje wanaimarisha uhusiano, ikiwemo kutekeleza Mpango Mkakati wa Mahakama wa 2015 hadi 2020. Tukio hilo limefanyika leo tarehe 17.05.2017 katika Ofisi ya Msajili iliyopo Mahakama Kuu jijini Dares Salaam.
Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ilvin Mugeta (kulia) akikabidhiana Mkataba wa Makubaliano ya Viwango vya Huduma Baina ya Mahakama na Kamisheni ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) na Kaimu Mkurugenzi kutoka Kamisheni ya Usuluhishi na Uamuzis(CMA)Bw. Shanes Nungu (kushoto).Mkataba huo una lengo la kuhakikisha kwamba Mahakama ya Tanzania na Wadau wa nje wanaimarisha uhusiano, ikiwemo kutekeleza Mpango Mkakati wa Mahakama wa 2015 hadi 2020.
No comments:
Post a Comment