Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe
Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akimkabidhi bendera Kapteni wa timu ya Azania
Khalid (katikati) ambayo inatarajia kusafiri kwenda nchini Uingereza kushiriki mashindano
ya kombe la Standard Chartered, kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko ya Fedha
za Kigeni wa Benki ya Standard Charted
Abdulrahman Said.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto)
akiongea katika hafla ya kukabidhi Bendera
ya Taifa Timu ya Mpira wa Miguu ya Azania inayoenda kuiwakilisha Tanzania
katika Michuano ya kombe la Standard Chartered nchini Uingereza, kulia ni
Balozi wa Uingereza nchini Bibi. Sarah Cooke.
Nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Azania Khalid Sultan akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa bendera iliyofanyika Jijini Dar es Salaam tayari kwa safari ya kuelekea nchini Uingereza kwa ajili ya Mashindano ya Kombe la Standard Chartered.
.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia)
akimkabidhi nyaraka za kusafiri mchezaji wa timu ya Azania tayari kwa ajili ya
kushiriki mashindano ya kombe la Starndard Chartered nchini Uingereza.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe
Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akimkabidhi vifaa vya michezo mchezaji wa timu
ya Azania Brian Mhapa tayari kwa ajili ya kushiriki mashindano ya kombe la Standard
Chartered nchini Uingereza.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa katika
picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Azania pamoja na uongozi wa benki ya
Standard Chartered baada ya halfa ya
kukabidhi bendera kwa timu hiyo tayari kwa mashindano ya kombe la Standard
Chartered nchini Uingereza. Picha Na Lorietha Laurence
*******************************************************
Na:
Genofeva Matemu – WHUSM
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Dkt. Harrison Mwakyembe ameikabidhi Bendera
ya Taifa Timu ya Mpira wa Miguu ya Azania inayoenda kuiwakilisha Tanzania
katika Michuano ya kombe la Standard Chartered nchini Uingereza.
Akizungumza
jana Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuiaga timu hiyo Mhe. Mwakyembe
amewataka vijana wa Timu hiyo kukumbuka kuwa ni muda wa kuonyesha uwezo na
vipaji walivyonavyo na kuvitumia kuiletea nchi heshima na kuitangaza katika
mataifa mengine duniani.
“Kuwa
mabingwa na kuweza kuiwakilisha Afrika Mashariki kuwania kombe la Standard
Chartered mmeonyesha uwezo wa hali ya juu, naamini mtatumia uwezo huo kufanya vizuri zaidi katika michuano hiyo.”Amesema
Mhe. Mwakyembe.
Kwa
upande wake Mjumbe wa Bodi ya Benki ya Standard Chartered Tanzania Balozi Ami
Mpungwe amesema kuwa Timu ya Azania ina uwezo kwani imefanya vizuri hapa
nyumbani katika michuano ya kitaifa na
kanda ya Afrika Mashariki ili kuhakikisha
wanapata ubingwa ambao umewawezesha kusonga mbele na kuitoa Kenya ambao ndio mabingwa watetezi.
Naye Balozi wa Uingereza Tanzania Mhe. Sarah Cooke
amewataka wachezaji hao kupambana kwa ari na uwezo mkubwa na kanda nyingine za nchi za Afrika
pamoja na mabara mengine wakiwa na lengo la kurejea nchini na ushindi ili
kuitangaza nchi yetu kupitia kombe la Standard Chartered.
Michuano
ya kuwania kombe la Standard Chartered inahusisha nchi zote ambazo Benki ya
Standard Chartered ina matawi ambapo kwa Tanzania Timu ya Azania inashiriki na
mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Mei 21 mwaka huu katika viwanja vya Anfield
nchini Uingereza.
No comments:
Post a Comment