KIUNGO wa kimataifa wa timu ya Yanga Thaban Kamusoko yupo chini ya uangalizi wa Daktari Nassor Matuzya kutokakana na maumivu yamguu aliyoyapa katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.
Akizungumza na mtandao huu, Dkt. Matuzya amesema kuwa Kamusoko alipata majeraha katika mchezo dhidi ya Njombe mji na kujitonesha katika mchezo na mtibwa katika uwanja wa uhuru ambapo hadi sasa hajaanza mazoezi,
"Kikubwa kinacho msumbua kamusoko ni kikombe cha ndani ya goti ambacho aliumia muda mrefu katika mchezo wao na Njombe mji ,kutoka na uwanja wanao chezea kwasasa umepelekea mushtua tena kidonda chake na tupo kwenye harakati za kumpatia matibabu,"alisema
Aidha Matuzya,alisema uwanja wa uhuru nichangamoto kubwa kwa wachezaji pia mbali na Kamusoko pia Donald Ngoma ameanza mazoezi mepesi na Amis Tambwe ambaye anaendelea vizuri na akitarajia kuwakabidhi kwa kocha kabla ya mchezo dhidi ya Kagera sugar
No comments:
Post a Comment